Staa wa Bongo Movie, Salim Ahmed ‘Gambo’.
Wema na Gabo.
Awali, mwanahabari wetu alihakikishiwa na msanii mmoja (jina
tunalihifadhi) kuwa kabla ya kuvuja kwa picha za sinema za Wema na Gabo
za filamu hivi karibuni, wawili hao waliwahi kuanguka dhambini miaka
kadhaa iliyopita.“Kwani unafiri ukaribu wa Wema na Gabo ni filamu tu? Kuna zaidi ya filamu, walishawahi kutoka miaka ya nyuma na ndio maana umeona hivi karibuni imekuwa rahisi tu kwao kufanya tena kazi pamoja,” alisema msanii huyo.
Baada ya kupata ubuyu huo, mwanahabari wetu alimtafuta Wema ili kuweza kumsikia anazungumziaje ishu hiyoi lakini bahati mbaya mrembo huyo hakuweza kupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, pia hakujibu. Alipoulizwa Gabo kuhusiana na madai hayo, alisema ukaribu wake na Wema umekuwa ukitafsiriwa tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye wanakutanisha zaidi na kazi tu na si vinginevyo.
“Mimi si mara moja au mara mbili. Wema nakutana naye, nakuwa karibu naye kwa ajiuli ya kazi. Umeona picha mpya za kimahaba hivi karibuni, zile ni za muvi tu,” alisema Gabo.
No comments:
Post a Comment