Sunday, 23 April 2017

Harmorapa: Sijawahi Kuachwa na Mwanamke

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmorapa amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hajawahi kabisa kuachwa na mwanamke bali yeye ndiye huwa anawaacha hivyo hajui suala la maumivu ya mapenzi.
Hamorapa akifanya yake ndani ya Dar Live hivi karibuni.
Harmorapa alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni  na kudai yeye hajui maumivu ya mapenzi kwa kuwa hajawahi kuachwa na mwanamke.
“Hapana mimi sijawahi kutoswa, kuachwa na mwanamke haijawahi kutokea kwangu, mimi ndiyo huwa nawaacha ila si kuachwa” alisema Harmorapa.

No comments:

Post a Comment