MALOVEE!
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na
wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’, kwa mara ya kwanza amevunja
ukimya na kufungukia penzi lake na modo anayedaiwa kufungwa nchini
China kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick
Cliff ‘Jack Patrick’.
Staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’.
Jux ambaye anasoma nchini China huku akifanya muziki wa Bongo Fleva,
alifunguka hayo juzikati katika ‘exclusive interview’ aliyoifanya na
mwanahabari wetu alipokuwa mjini Kahama alipokwenda kwenye Serengeti
Fiesta 2014.