Jaja Vs Zahir ni shiida, Maximo awaamua mara 3

Beki Rajab Zahir (kulia) dhidi ya Genilson Santos ‘Jaja’ (kushoto), wamekuwa na kazi ya ziada mazoezini.KWELI Yanga imepania kufanya kweli, kila mchezaji anataka kuonyesha uwezo wa juu, lakini ushindani huo umesababisha upinzani kuwa mkali kwa wachezaji wa timu hiyo, beki Rajab Zahir dhidi ya Genilson Santos ‘Jaja’, ambapo wamekuwa na kazi ya ziada mazoezini.
Jaja,
raia wa Brazil, ameonekana kupata wakati mgumu kila anapokuwa akikabwa
na Zahir kiasi cha kufikia wawili hao kukwaruzana zaidi ya mara moja
katika siku tofauti, hali ambayo imesababisha kocha wao mkuu, Marcio
Maximo kuingilia na kuwapa maelekezo zaidi ya mara moja pia.
Katika
mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Shule ya
Sekondari ya Loyola jijini Dar, Jaja alionyesha ufundi lakini Zahir
alikuwa mgumu na hakutaka kukubali kupitwa kirahisi, hali hiyo
ilisababisha kuchezeana kibabe mara kadhaa, ambapo kuna muda alimkwatua
kiasi cha Jaja kutolewa nje na kupatiwa huduma ya kwanza.
Jana pia kwenye Viwanja vya Tanganyika
Packers, Kawe jijini, Zahir alipewa jukumu la kumdhibiti Jaja ambapo
shughuli ilikuwa pevu, baada ya muda mambo yakawa kama ya juzi.
Wakiwa katikati ya mazoezi, Zahir alimkwatua Jaja kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kitendo kilichosababisha Jaja kukasirika na kumvaa beki huyo, lakini kabla ya kumfanya chochote, Maximo aliingilia na kusimama kati yao kisha kuanza kutoa maelezo kwa wote wawili.

No comments:
Post a Comment