Monday, 28 July 2014

vituko mtaan CHEKI NGUMI JIWE

MKUDE SIMBA - MTOTO WA MKUDE (SIMBA SWAHILI AUDIO COMEDY)

MKUDE SIMBA - DIAMOND PLATNUMZ (SWAHILI AUDIO COMEDY)

MKUDE SIMBA - MTOTO WA MKUDE (SIMBA SWAHILI AUDIO COMEDY)

MKUDE SIMBA - YUPO BRASIL (SWAHILI COMEDY AUDIO)

MKUDE SIMBA - MAPERA (SWAHILI COMEDY AUDIO)

Jack Wilshere ajutia uvutaji sigara.






Liverpool yamsajili Divorc Origi


Divorc Origi katika mojawapo ya mechi za Ubelgiji

Boko Haram wazilenga Nigeria na Cameroon



Boko_haram

Kombora lalipua matenk ya mafuta,Libya


Vikosi vya zima moto vya Libya vinapambana kujaribu kuuzima moto baada ya kombora la roketi kulipua tanki la kuhifadhia mafuta wakati wa mapigano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mji mkuu Tripoli. Tanki hilo ni miongoni mwa matanki yanayomilikiwa na Kampuni ya mafuta ya serikali ya Libya yenye lita milioni sita za mafuta.
Msemaji wa Kampuni hiyo Mohamed Al-Hariri amesema iwapo moto huo utasambaa kwenye matanki mengine ya karibu huenda ukasababisha madhara makubwa katika eneo lenye upana wa kilomita tano.
Serikali ya muda ya Libya imetaka ustishaji wa mapigano katika eneo hilo la maafa ili kuruhusu vikosi vya zima moto kufanya kazi yao bila kuingiliwa.

JOHARI AKANUSHA MADAI YA KUBATIZWA

MKONGWE wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amedaiwa kubatizwa juzikati katika Kanisa Katoliki Nyalikungu wilayani Maswa, Simiyu lakini mwenyewe amekanusha.
Mkongwe wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
Chanzo makini kilichodai kushuhudia ubatizo, kilieleza kuwa Johari alifika Jumapili kanisani hapo na watu kuhoji kwa nini achelewe kubatizwa? Alipotafutwa na mwanahabari wetu, Johari alitiririka:
“Kweli nilikwenda kwenye hilo kanisa lakini sikubatizwa kama alivyosema huyo mtu. Nitabatizwaje mara mbili? Mimi nilishabatizwa tangu utotoni.”

Sunday, 27 July 2014

Hii ndio ratiba ya Fiesta 2014 kwa Kanda ya Ziwa

Hii ndio ratiba ya Fiesta 2014 kwa Kanda ya Ziwa: Kama ulimiss basi ile ratiba ya tamasha la fiesta iliyotolewa hapo jana kupitia xxl, wakati mkurugenzi wa vipindi Clouds Fm bwana Sebasti...

Tazama Interview ya alikiba ndani ya XXL

 Tazama Interview ya alikiba ndani ya XXL: Leo hii Alikiba alikuwa ndani ya Crazy Friday ya XXL kutambulisha single zake mbili "Kimasomaso" na "Mwana" fan...

Brand New Video: Wahalade - Barnaba

 Brand New Video: Wahalade - Barnaba: Ile video mpya ya Barnaba "Wahalade" niliyokuhabarisha kuwa video queen wake ni mke wake mwenye a.k.a Mama Steve, hii hapa ndo ...

Diamond Platnumz awachapa vibaya akina 2 face


Diamond Platnumz ambaye yuko Marekani katika Tuzo za Afrimma Awards ambazo zimefanyika leo jijini Texas asubuhi kule ni kama saa saba za Usiku na ameibuka mshindi kwa kunyakua Tuzo Mbili moja ni Msanii bora wa East Africa 
(Best Male East Africa
ambapo alikua akichuana na
Ben Pol (Tanzania)
Bebe Cool (Uganda)
Wyre (Kenya)
Navio (Uganda)
Jackie Gosee (Ethiopia)


wimbo bora wa kushilikiana 
(Best Collabo
na kuzigaragaza ngoma kama
2face ft Tpain- Rainbow ( Nigeria/ United States)
Mafikizolo ft Uhuru-- Khona ( South Africa)
Dr Sid ft Don Jazzy /Phyno/Wizkid- Surulere remix(Nigeria)
Amani ft Radio and Weasel – ‘Kiboko Changu’ (Kenya/Uganda)
Jmartins ft DJ Arafat--- Touching body ( Nigeria/ Ivory Coast)
R2bees and Wizkid- Slow down ( Ghana/ Nigeria)

Hii ni orodha kamili ya washindi wa AFRIMMA 2014

Hii ni orodha kamili ya washindi wa AFRIMMA 2014
Best DJ Africa 2014- Dj Black (Ghana)
 Best African DJ USA 2014 – Dj Josh (Kenya)
 Best Video of the Year 2014- Flavour (Nigeria)
Best Male East Africa 2014- Diamond (Tanzania)
 Best Male West Africa 2014- Davido (Nigeria)
 Best Female East Africa 2014- Lady Jaydee (Tanzania)
 Best Female West Africa 2014 – Tiwa Savage (Nigeria)
 Best Male Central Africa 2014 – Fally Pupa (Congo)
 Best Female Central Africa 2014- Gasha ( Cameroon)
 Best Male Southern Africa 2014- Khuli Chana (South Africa)
 Best African Group 2014- P-square (Nigeria)
 Best Male Diaspora 2014- Fuse ODG (Ghana)
 Best Female Diaspora 2014- Les Nubians (Cameroon)
 Best Female Southern Africa 2014- Zahara (South Africa)
 Best Dancehall Artist 2014 – Timaya (Nigeria)
 Best Dance in a Video 2014- Iyanya (Lekwa Ukwu) (Nigeria)
 Best Gospel Artiste 2014- Bahati (Kenya)
 Best Traditional Artist 2014- Flavour (Nigeria)
 Best Newcomer 2014- Stanley Enow (Cameroon)
 Best Video Director 2014- Ogopa Dj’s (Kenya)
 Music Producer of the year 2014- Dj Oskido (South Africa)
 Best Dance Group 2014- Imagineto (Nigeria)
 Best Rap Act 2014- Sarkodie (Ghana)
 Best Collaboration 2014- Mafikizolo ft Uhuru (Khona) (South Africa)
 Song of the Year 2014- Kcee (Nigeria)
 Artist of the Year 2014- Davido (Nigeria)
 Leadership in Music Award 2014- (2face Idibia)
 Legendary Award 2014- (Yvonne Chaka Chaka)
 Transformational Leadership Award 2014- (Chief Dr. Godswill Akpabio)


Arsenal kumsajili Calum Chambers

wachezaji wa Arsenal
Kilabu ya Uingereza ya Arsenal inakaribia kumsajili mlinzi wa kilabu ya Southampton Calum Chambers kwa takriban paundi millioni 16.
Mchezaji huyo wa timu ya Uingereza isiozidi umri wa miaka 19 alifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya ijumaa.
Chambers mwenye umri wa miaka 19 ameshiriki mara 25 katika timu ya soka ya taifa la Uingereza na kwamba Arsenal inamuona kama suluhu wa safu ya ulinzi wa kulia na katikati .
Arsenal pia inamsaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliichezea timu ya Ufaransa katika kombe la dunia.

BAHATI BUKUKU APATA AJALI.

Bahati Bukuku apata AJALI
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku amepata ajali ya gari akiwa na dereva wake, Eddy maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Akiongea kwa simu Bahati amesema: “Ni Mungu tu aliyetuokoa, tulikuwa tunaelekea Kahama kwenye huduma ghafla tukagongana uso kwa uso na lori, gari yetu aina ya Toyota Nadia  iliruka na kubiringika kama mara tatu hivi, tumetoka tukiwa tumeumia sana.
“Hapa siwezi kusimama wala kukaa na dereva wangu kaumia sana mguu. Gari yangu imeumia sana wala huwezi kuamini kama kuna mtu katoka salama.”
Taratibu za kumhamishia Bahati kutoka Hospitali ya Kongwa kuja Muhimbili zinafanywa na ndugu pamoja na marafiki.
Tunakuombea upone haraka Bahati.

Shuwari itaendelea zaidi Gaza?

Watoto wa Gaza
Afisa wa serikali amesema kuwa Israel iko tayari kuzidisha kipindi cha kusitisha mapigano Gaza kwa saa kadha.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 12 yanatarajiwa kumalizika baada ya saa 2 za usiku za Afrika Mashariki.
Afisa huyo alisema muda huo huenda ukazidishwa kwa saa nne hadi usiku saa sita za Mashariki ya Kati.
Baraza la usalama la Israel linatarajiwa kukutana usiku.
Wakuu wa afya wa Gaza wanasema raia zaidi ya 1,000 wa Palestina, wengi raia, wameuwawa tangu mapigano ya sasa baina ya Israel na Hamas kuanza.
Maiti zaidi ya 80 zimekutikana chini ya vifusi wakati mapigano yaliposita.
Wanajeshi 40 wa Israeli wamekufa, pamoja na raia wawili na mfanyakazi kutoka Thailand.
Wakaazi wa Gaza wameingia mabarabarani kuchukua nafasi ya hali ya shuwari iliyopatikana.

UPENDO NKONE APONEA CHUPU CHUPU KULAANIWA NA BIBI YAKE


UKISIKILIZA wimbo wake wa Hapa Nilipo, Usinipite Bwana, Usifurahi Juu Yangu na Upendo wa Yesu, hakika utagundua kwamba kuna kitu Mungu amekiweka katika ubongo wa mwimba  wa nyimbo za Injili mahiri nchini, Upendo Nkone.
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Nkone.
Ana sauti nzuri, nyimbo zake zinagusa wengi kutokana na ujumbe mzito ambao Mungu amemtumia ahubiri Injili kwa watu wote, kila mmoja kwa nafasi yake anaguswa kumsikiliza.
Exclusive Interview imezungumza naye mambo mengi kuanzia maisha yake ya utotoni hadi alipofikia hatua ya kuwa mwimbaji mkubwa wa muziki wa Injili nchini kwa mtindo wa maswali na majibu kama ifuatavyo:
Mwandishi: Wasomaji wetu wangependa kujua historia yako japo kwa kifupi.
Upendo: Mimi ni mzaliwa wa Kijiji cha Bitale mkoani Kigoma, ni mtoto pekee wa kike na wa kwanza kati ya watoto saba, ni mkristo, nimekua na kulelewa katika maisha ya dini, babu yangu mzee Nkone akiwa ni Askofu wa Kanisa la Pentekoste (PFTC).
Ni mama mwenye watoto 6, wawili wakiwa wangu wa kuzaa, wanne wa mume wangu mpendwa aliyenioa baada ya kufariki mume wangu wa kwanza na yeye kufiwa na mkewe.
Nimemaliza masomo ya msingi na sekondari ingawa sikufanya vizuri lakini baadaye nilijiunga na chuo cha ufundi wa ushonaji cha FDC kilichopo mkoa wa Pwani, baada ya hapo maisha yaliendelea kusonga kama kawaida, nikafanikiwa kupata mume.
Mwandishi: Kitu gani unakikumbuka wakati ulipokuwa shuleni?
Upendo: Nilikuwa na tabia ya udokozi, nilikuwa naiba fedha nyumbani naenda kula maandazi shuleni wakati huo nilikuwa niko darasa la nne.
Mwandishi: Nani alikufundisha udokozi au ni tabia yako ya asili?
Upendo: Hapana kuna mmoja wa ndugu zangu ambaye alikuwa ananizidi umri ndiye alikuwa ananituma, baadaye tunagawana na kusema eti tumeokota, mchezo huo uliendelea kwa muda mrefu sana, kila wakiacha fedha nyumbani mimi nazipitia.
Mwandishi: Ukiachana na tukio hilo, unaweza kutupa tukio lingine unalolikumbuka la udokozi?
Upendo: Kuna siku ambayo siwezi kuisahau, niliiba fedha ya sadaka (fungu la kumi) ambayo bibi alikuwa katunza chini ya godoro lake kwa ajili ya kupeleka kanisani,
ila wakati naichukua ile bahasha nilikuwa na mashaka kwa namna fedha  zilivyokuwa zimewekwa kiasi kwamba hata wewe ungejua zimewekwa kwa kazi maalumu, ila kwa kichwa ngumu nikachukua tu.
Mwandishi: Haukushtukiwa?
Upendo: Bibi alikuwa ananipenda sana, mbaya zaidi badala ya kunihisi, aliniita na kunishitakia kuwa kaibiwa fedha yake ya sadaka na kunieleza kwamba inamuuma sana kwa sababu alipanga akamtolee bwana fungu la kumi. Ilikuwa ngumu kujitangaza ama kumrudishia moja kwa moja kwa sababu ningepigwa na ingekuwa ni aibu kwangu lakini pia mimi ndiye niliyekuwa mjukuu wake kipenzi, ningemuumiza sana.
Mwandishi: Kwani ni zilikuwa shilingi ngapi ulizokwapua?
Upendo: Kama elfu kumi kwa kipindi hicho ilikuwa na thamani kubwa kuliko sasa, bibi alikuwa anafanya biashara zake ndogondogo za kuuza mikate na mkaa tena mimi ndiye nilikuwa muuuzaji mkuu, utoto jamani! (anacheka na kusikitika kidogo).
Mwandishi: Bibi alichukua hatua gani sasa kwa kuibiwa fedha hiyo?
Upendo: Alitangaza sana kwa mtu aliyeichukua airudishe bahasha yake kwani aliweka sadaka kwa ajili ya kupeleka kanisani, baada ya kuona kimya alitangaza kutoa laana kwa aliyechukua kwa kuiba lakini kama aliiokota hatapatwa ila ni vizuri kuirejesha.
Nikaingiwa na huruma, nikamwambia twenda nikamsaidie kuitafuta, tukaingia ndani na kuanza kuitafuta baadaye nikamwambia aangalie upande wa pili wa kitanda alipoinama nikaiweka upande mwingine nikajifanya natafuta kisha nikamwambia bibi hii hapa, akaja akaichukua ila alishangaa, hivyo ndivyo nilivyofanya.
Je, Upendo Nkone alikwepaje hiyo laana mpaka sasa anaendelea kuimba na kupeta katika kumtukuza Mungu muumba mbingu na nchi? Fuatilia Jumamosi ijayo.

Saturday, 26 July 2014

ALI KIBA, DIAMOND WATATOANA ROHO!

Na Sifael Paul
Hatimaye! Kwa mara ya kwanza staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba ameibuka na kumlipua hasimu wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hali inayotafsiriwa kwamba bifu lao sasa limefika pabaya ikidaiwa kwamba wanagombea nyota (ustaa).
Staa ‘the big name’ wa Bongo Fleva ndani na nje ya Bongo, Ali Saleh Kiba.
Kupitia Kipindi cha The Sporah Show, usiku wa Jumanne wiki hii kwenye CloudsTV, Kiba alimchakaza Diamond ambapo alifunguka mengi ikiwemo chanzo cha ugomvi wao.
Kiba alizungumzia sosi iliyotengeneza bifu kati yake na Diamond ambapo aliulizwa kama ana namba ya simu ya msanii huyo ndipo akatiririka:
“Nilikuwa nayo kipindi fulani, nilipohisi amenikosea nikaona sina ulazima wa kuwa nayo.
“Kuna kipindi alinikosea kwa sababu nilisikia amesema kwamba tulirekodi wote ule Wimbo wa Single Boy, jambo ambalo halikuwa kweli. Halafu akasema mimi ndiyo nilimfuta.
Staa wa muziki Bongo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’,
“Diamond alinikosea kwa sababu kutokana na mimi ndiye nilifanya wimbo wake wa Lala Salama ambao upo kwenye album yake, akanifuta nikahisi amenikosea sana nilichoimba mimi akawa ameimba yeye, alichoniomba nifanye nilifanya kwa mapenzi yote na mimi namsapoti kila msanii wa Tanzania anayefanya vizuri, sikatai anaimba vizuri, sijui ukisema amekopi, mimi sijamaindi wala nini lakini usiseme kwa watu ukadanganya nikaonekana mimi sifai, siko hivyo mimi.
“Watu wengine ambao hawaelewi vizuri wanaweza wakamwamini Diamond, kila mtu ana mapenzi yake labda kuna wengine wanampenda Diamond wengine wanampenda Ali Kiba. Wanaweza wakawa wengine wanampenda Diamond wakaamini mimi nilimfuta kwenye wimbo wangu wa Single Boy lakini mimi wala, shahidi yangu ni produyuza Manecky (AM Records) kwani ndiye alitengeneza ule wimbo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael 'Lulu'
“Sikuwahi kwenda studio na Diamond, sikuwahi kufikiria kufanya wimbo naye. Ila alinipigia simu baada ya ule wimbo wa Single Boy kuvuja. Akaomba afanye na mimi, akanipa hadi idea (wazo) ya video, nikamwambia nimeshafanya na Jaydee (Judith Wambura).
Nikamwambia itapendeza zaidi tukifanya wimbo mwingine kwa sababu hii tukifanya mimi na wewe haita-make sense (haitaeleweka), inapendeza ikiwa single boy na single girl, hicho ndicho kitu nilimjibu.
“Baada ya kama wiki moja nikasikia kwenye mablog, nikapigiwa simu kwamba mimi nimemfuta Diamond kwenye ule wimbo wakati yeye ndiye aliyenifuta katika wimbo wake, shahidi prodyuza wangu KGT.
“Kutoka hapo nikaona hakuna tatizo lakini kwa kujua yeye alinifuta katika wimbo wake. Mimi siyo shabiki wa Diamond ni shabiki wa muziki mzuri. “Kuna watu wanasema kachukua kiti changu? Labda kama ni kiti ambacho nilikuwa nimekaa kina vumbi na ninachotakiwa ni kukipangusa tu na kukaa tena, labda yeye yuko siti nyingine ila ya nyuma.
“Niliambiwa alisema vitu vingi, mara nilikopa fedha benki ili nimalizie nyumba na mambo kama hayo so siwezi kufanya naye kazi.” Baada ya Kiba kumchakaza, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond naye alijibu mapigo bila kutaja jina la Kiba ambapo aliandika: “Tatizo lako wewe unawaza kushindana na mimi ili nishuke…Wakati mwenzako nawaza kushindana na watu wa mataifa mengine ili nilete sifa na heshima nchini kwetu.”
Hata hivyo, baada ya hayo yote kuliibuka madai kwamba mbali na ishu za muziki, mastaa wa kike wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu wanahusishwa kwenye gogoro hilo kisa wivu wa kimapenzi hivyo ishu hiyo bado ni mbichi. Tusubiri mwisho WAKE!

Tambwe na mgomo baridi Simba SC

Straika wa kimataifa wa ya Simba, Mrundi, Amissi Tambwe,
Martha Mboma na Ibrahim Mussa
BAADA ya siku nne kutoonekana mazoezini imebainika kuwa straika wa kimataifa wa ya Simba, Mrundi, Amissi Tambwe, alikuwa na mgomo baridi akiushinikiza uongozi kumlipa fedha zake za usajili.
Awali iliripotiwa kuwa straika huyo aliyefunga mabao 19 msimu uliopita na kunyakua kiatu cha dhahabu, alikuwa amefiwa na shangazi.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo kilisema kuwa, mshambuliaji huyo aliamua kususia mazoezi akishinikiza kumaliziwa fedha zake za usajili alizokuwa akiidai timu hiyo.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hata hivyo mchezaji huyo amelipwa pesa yake, kilichobaki kwa sasa ni kuongezewa mshahara na marekebisho kadhaa katika mkataba wake na wamemuahidi kuanza kumlipa mwakani ndiyo maana juzi Alhamisi alianza mazoezi.
“Tambwe alikuwa na mgomo wala hakusafiri kama ilivyodaiwa, alikuwa kalala tu nyumbani kwake tangu Jumamosi iliyopita akishinikiza kumaliziwa fedha zake za usajili, kapewa chake ndiyo maana unamuona mazoezini,” kilisema chanzo hicho.

 DAVINA APEWA KIPIGO KIKALI NA MUMEWE.


KIBANO! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ anadaiwa kupewa kipigo kikali na mumewe, muda mfupi baada ya kukutwa akiongea kimahaba na simu iliyodaiwa kupigwa na mwanaume mwingine.
Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’
Tukio hilo lilitokea nyumbani kwa msanii huyo, Mbezi-Beach, Dar, Julai 22, mwaka huu ambapo Davina alikutwa akizungumza na mwanaume ambaye haikujulikana mara moja ni nani ndipo mumewe alipomshushia kipigo ‘hevi’.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu familia hiyo, mume wa Davina aliibua timbwili hilo baada ya kumsikiliza kwa makini mkewe huyo na kugundua anazungumza na mwanaume mwingine wakiahidiana kitu f’lani.
“Mumewe alitega sikio kwa makini na kugundua alikuwa akizungumza na mwanaume, akamsogelea karibu na kunasa mazungumzo yao, akamuoma simu mara moja, Davina akaanza kujitetea ndipo mtiti ulipoibuka, mume akaanza kumpiga mke ingawa hakumuumiza kiivyo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya data hizo kutua kwenye Dawati la Risasi Jumamosi, mwanahabari wetu alimvutia waya Davina ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kufafanua kuwa hakuwa akiongea na mwanaume huyo kwa lengo baya zaidi ya maongezi ya kikazi.
“Dah! Umejuaje hii ishu ni ya kifamilia hivyo! Mmh...kweli ninyi ni noma, anyway ishu ni kwamba, mume wangu alinifuma nikiongea na simu ya jamaa mmoja ambaye alikuwa ananipigia ili anipatia fedha zangu ambazo zilibaki baada ya kufanya tangazo moja linalohusiana na mambo ya Ukimwi.
“Wakati naongea, yeye (mumewe) hakujua nini kinaendelea zaidi alikuwa akisikia sauti ya mwanaume tu na majibu yangu kweli akajikuta amepaniki na kunivaa akiwa ana hasira, si unajua mtu yeyote anayekupenda wivu huwa ni kitu cha kawaida tu lakini nilimwelewesha baadaye akanielewa na maisha yanaendele kama kawaida,” alisema Davina.

SHEKHE MKUU ATANGAZA SWALA YA IDD KITAIFA

  Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametangaza Swala ya Sikukuu ya Idd El Fitri inayotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa wake.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao maalumu katika Ofisi za  Mkoa wa Dar es Salaam za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) hii leo, Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo sambamba na hotuba mbalimbali inatarajiwa kufanyika saa moja asubuhi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar kutegemea na siku ya Idd itakapodondokea ambapo inatarajiwa kuwa siku ya Jumatatu Julai 28 au Jumanne  Julai 29 mwaka huu.
Shekhe Alhad alisema kuwa swala hiyo itahudhuriwa na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Tanzania, Jakaya Kikwete na viongozi mbalimbali wa Kiislamu na wa kitaifa ikifuatiwa na Baraza la Idd litakalofanyika saa 9 Alasiri katika Viwanja vya Karimjee, Dar ambapo Mgeni Rasmi wa Baraza hilo atakuwa ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Peter Pinda.



IMETOKA GLOBAL PUBLISHERS

MWANAUME AZAMISHWA SHOKA KICHWANI

Na Mwandishi Wetu

NI tukio la kutisha! Tukio hilo linadaiwa kutokea jijini Mwanza ambapo mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja) amepigwa shoka la upande wa kushoto wa kchwa na kuzama ndani ikidaiwa ni sababu ya kufumaniwa.
Mgonjwa akiwa wodini na shoka kichwani.
Picha za tukio hilo zilitumbukizwa mitandaoni na mtu anayedaiwa ni daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji mtuhumiwa huyo.
TAARIFA FUPI

Kwenye mitandao ya kijamii, picha hizo ziliambatana na maelezo mafupi sana kwa…
Na Mwandishi Wetu
NI tukio la kutisha! Tukio hilo linadaiwa kutokea jijini Mwanza ambapo mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja) amepigwa shoka la upande wa kushoto wa kchwa na kuzama ndani ikidaiwa ni sababu ya kufumaniwa.
Mgonjwa akiwa wodini na shoka kichwani.
Picha za tukio hilo zilitumbukizwa mitandaoni na mtu anayedaiwa ni daktari aliyekuwa akimfanyia upasuaji mtuhumiwa huyo.
TAARIFA FUPI
Kwenye mitandao ya kijamii, picha hizo ziliambatana na maelezo mafupi sana kwa chini yakisomeka hivi:
“Baada ya madoctor (madaktari) wa Bugando kupambana kuokoa maisha ya jamaa aliyefumaniwa huko Mwanza hatimaye wamefanikiwa kumtoa shoka kichwani na hali yake bado mbaya, yuko ICU (chumba cha wagonjwa mahututi) kwa uangalizi zaidi. Mke wa mtu sumu!”
MAZINGIRA YA PICHA
Kwenye baadhi ya picha, mwanaume huyo anaonekana ana nywele ndefu kidogo na mustachi ulionona. Picha nyingine zinamuonea akiwa na kipara nusu kichwa baada ya kunyolewa nywele ili madaktari waweze kumfanyia upasuaji wa kulitoa shoka hilo lililozama ndani sana.
MAZINGIRA YA HOSPITALI
Baadhi ya watu waliochangia kwenye mitandao ya kijamii walisema tukio hilo lilitokea nje ya Tanzania. Walisema ingekuwa Bongo lazima vyombo vya habari vingeandika lakini hata hivyo, mazingira ya chumba cha upasuaji alicholazwa mwanaume huyo yalionesha ni Tanzania.
Shoka likiwa limetolewa na madaktari wa upasuaji.
KWA NINI NI TANZANIA?
Ni Tanzania kwa sababu, picha zinamuonesha mwanaume huyo akiwa kwenye kitanda cha chumba cha upasuaji akiwa amefunikwa shuka yenye maandishi yanayosomeka kwa kifupi MSD.
MSD ni kifupi cha maneno Medical Stores Department (Bohari Kuu ya Dawa). Mbali na kugawa dawa katika hospitali za serikali nchini, pia MSD inatoa mashuka yenye nembo hiyo kwa ajli ya kujifunika wagonjwa mahospitalini.
RPC ASHTUKA
Ili kupata ukweli wa madai hayo kwamba mwanaume huyo alikutwa na mkasa huo mkoani Mwanza na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Risasi Jumamosi liliingia kazini kufuatilia tukio hilo kwa kuzungumza na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime na kumuuliza kama ana ishu hiyo mezani kwake.
“Mh! Hivi nyiye mnajua kama mitandao siku hizi imezua balaa kubwa sana? Hivi tukio kama hilo, mwanaume apigwe shoka mpaka kuzama kichwani, alazwe Bugando Hospital mimi nisijue?
“Hakuna kitu kama hicho.
Hayo ni mambo ya mitandao tu, sijui wametoa wapi? Halafu si umeona hata maelezo hayajitoshelezi? Mimi mkoa wangu upo shwari kabisa mpaka hivi ninavyoongea na wewe,” alisema Afande Fuime kwa sauti iliyoashiria kushtuka.
Picha ya X-Ray shoka lilivyoingia pichani.
DAKTARI BUGANDO AONGEA
Ili kuchimba zaidi, Risasi Jumamosi lilimtuma paparazi wake aliye Mwanza, Mashaka Bartazal ambaye alikwenda hadi Hospitali ya Rufaa, Bugando na kuzungumza na daktari mmoja anayefanya kazi kwenye kitengo cha upasuaji ambapo alisema:
“Ni kweli tunapokea watu wenye matukio ya kutisha lakini mwanaume aliyepigwa shoka mpaka likazama kichwani hatujampokea,” alisema daktari huyo akiomba asitajwe jina gazetini kwani si msemaji wa hospitali hiyo.
UKIO LAHAMISHIWA KAHAMA
Katika hali iliyozidi kuibua maswali, baadhi ya watu waliozungumza na mwandishi wetu wa Mwanza walisema wamesikia mwanaume huyo alikumbwa na balaa hilo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
RISASI JUMAMOSI KAHAMA
Kwa sababu Kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa Bongo ina waandishi nchi nzima, ilimwagiza mwandishi wake aishiye Kahama kulisaka tukio hilo na kutoa ripoti Makao Makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar ambapo alifanya hivyo kwa kuomba apewe saa mbili tu kufuatilia.
Baada ya saa mbili kupita, mwandishi wetu alitoa ripoti makao makuu kwamba, hakuna mwanaume aliyelazwa kwenye hospitali yoyote ya wilayani Kahama wala mkoa huo kwa kupigwa shoka la kichwani.
MASWALI YA MSINGI
Bado jamii imebaki na maswali kadhaa ya kujiuliza. Kwamba, kama ni tukio la Tanzania, hiyo sehemu aliyolazwa mtu huyo hakuna jeshi la polisi? Kwa sababu polisi ndiyo wanahusika na kupewa taarifa za matukio kama hayo na kuyatangaza.
Pili, jamii inauliza kwamba, inawezekana mwanaume huyo baada ya tukio hakupitia au kupitishwa polisi kwa ajili ya kupewa Police Form No. 3 (PF3)?
Kama ni hivyo, hospitali walimpokeaje mtu wa hivyo hasa ikizingatiwa kuwa, hali yake ilionekana ni mbaya kwani hata picha ya X-Ray ilionesha shoka hilo lilizama kiasi cha kama inchi sita kwenda ndani na kubakiza kidogo kutokea upande wa kulia wa kichwa.
UKWELI BADO UNATAFUTWA
Bado Magazeti Pendwa ya Global Publishers (Uwazi, Risasi, Ijumaa, Amani na Ijumaa Wikienda) yanaendelea kuchimba tukio hilo ambalo limeonekana kuishtua sana jamii.



IMETOKA GLOBAL PUBLISHERS

Hatari

KIJANA ANG'OLEWA MENO 232 NCHINI INDIA


Madaktari wakikagua meno aliyong'olewa kijana Ashik Gavai (17).
MADAKTARI nchini India wametumia saa saba kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai (17) aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kichwa.

Meno aliyong'olewa kijana Ashik Gavai (17).
Dk. Sunanda Dhiware, Mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo na tindo kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba hilo ni tukio la ajabu na linaingia katika rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha jopo la madaktari wanne.
DK. Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna hiyo.
Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu ya maumivu na kwamba walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na ndipo wakamleta Mumbai.
Chanzo: BBC

Mourinho : Drogba ni Chelsea damu

Mourinho : Drogba ni mChelsea damu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .
Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 36 aliwahi kushinda mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia mwaka wa 2004-2012 kabla ya kuguria Galatasaray.
"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na timu kwa jumla''.
Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .
Drogba akiwa Galatasaray.
Aliondoka Stamford Bridge mwaka wa 2012 baada ya kutinga penalti iliyoisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich .
Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013.

Marekani yafunga Peace Corps Kenya

Marekani yafunga huduma ya Peace Corps nchini Kenya
Shirika la Marekani la kutoa misaada ya matibabu US Peace Corps limetangaza kuwa linasitisha shughuli zake zote nchini Kenya.
Shirika hilo limeamuru kuondolewa kwa wafanyikazi wake wote zaidi ya hamsini nchini humo.
Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na tashwishi kuhusu usalama nchini Kenya kufuatia msururu wa mashambulizi yaliyotekelezwa na makundi ya wanamgambo kutoka Somalia Al shabab na washirika wake.
Marekani majuzi ilikuwa imetangaza kupunguzwa kwa idadi ya wafanyikazi katika balozi yake iliyoko mjini Nairobi.
Balozi hiyo ni mojawepo ya maeneo yaliyoshambuliwa mwaka wa 1998 na washirika wa Al Qaeda nchini Kenya.
Polisi wakishika doria Pwani ya Kenya
Aidha ripoti hiyo inawadia siku mbili baada ya Shirika linalosimamia usafiri wa Anga ya Marekani kupiga marufuku safari zote za ndege katika anga ya Kenya.
Hatua ya shirika la US Peace Corps kuwaondoa wafanyikazi wake kutoka Kenya imechukuliwa muda mfupi baada ya wanawake watatu kutiwa nguvuni nchini Marekani na Uholanzi kwa madai ya kutoa ufadhili kwa kundi la
wanamgambo wa kiislam wa al-Shabab nchini Somalia .
Wizara ya sheria nchini Marekani imesema kuwa mwanamke mmoja alitiwa mbaroni alipokuwa nyumbani kwake katika jimbo la Virginia na mwingine alishikwa mjini Washington.
Washukiwa hao wanadaiwa kutuma pesa katika mtandao wa malipo madogo madogo kila mwezi.
Kundi la Al shabab limekuwa likitekeleza mashambulizi ndani ya Kenya
Marekani ililitangaza kundi la al-Shaabab kuwa kundi la kigaidi mwaka 2008.
Wizara ya sheria ya Marekani imesema kuwa washukiwa wengine wawili akiwemo Jama Mohammed Fardowsa wamejificha nchini Kenya na Somalia.
Maafisa nchini Kenya wamesema bado hawajapata habari kuhusu kuwepo kwa Bi. Fardowsa nchini humo.
Huku hayo yakiarifiwa Polisi nchini Kenya wanasema kuwa mtalii wa kike ameuwawa kwa kupigwa risasi katika mji wa Mombasa lakini wamesema kuwa bado hawana uhakika iwapo mauaji hayo yanahusiana kwa vyovyote na mashambulizi ya hivi karibuni yaliyotekelezwa na al shabaab.

Straika wa England atua Yanga, aanza mazoezi

Na Sweetbert Lukonge
YANGA kweli ngoma inogile! Ndivyo unaweza kusema, baada ya mshambuliaji mwingine kutua klabuni hapo akitokea England na kisha kuanza mazoezi chini ya Kocha Marcio Maximo.
Mshambuliaji mpya wa Yanga aliyekuwa akikipiga katika timu ya Coventry City ya England Suleiman Abdallah Mbarouk.
Mshambuliaji huyo raia wa Tanzania ambaye amekuwa akicheza soka England kwa miaka mingi, Suleiman Abdallah Mbarouk, aliyekuwa akikipiga katika timu ya Coventry City ya England inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, alijumuika mazoezini kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini lakini bado hajapewa mkataba wowote.
Taarifa kutoka klabuni hapo zinaeleza kuwa, Maximo amekabidhiwa mchezaji huyo kwa ajili ya kumfanyia majaribio na kama akionekana anaweza, atapewa mkataba.
Championi Ijumaa, lilizungumza na mchezaji huyo ambapo alisema amerejea nchini kwa kuwa mkataba wake na klabu yake nchini England ulimalizika na hakuwa kwenye mipango ya timu yoyote.
Suleiman Abdallah Mbarouk akiwa na Jaja.
“Nimeachana na Coventry City mwaka mmoja hivi uliopita, niliumia mgongo, hivyo nikawa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita, lakini hivi sasa nimepona, nahitaji kuendeleza kipaji changu cha soka.
“Wakala wangu, anaitwa Salim ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Afri-Soccer cha Zanzibar, ndiye amenileta hapa kwa ajili ya majaribio, nilianzia Simba na sasa nimekuja kujaribu Yanga.”
Mchezaji huyo ambaye alisema kabla ya kutua Coventry City aliwahi kupata mafunzo ya soka katika kituo cha Chelsea cha England, hakuonyesha uwezo mkubwa katika mazoezi ya jana, hata Maximo pia hakutaka kuzungumza chochote juu yake.
Gazeti hili lilipotafuta takwimu na rekodi zake lilibaini kuwa aliwahi kuichezea timu ya watoto ya  Coventry City, lakini kama anahitaji kupata nafasi kweli kwenye kikosi cha Yanga, basi kazi kubwa ipo mbele yake.





IMETOKA GLOBAL PUBLISHERS

Drogba arejea CHELSEA.


DIDIER DROGBA AREJEA CHELSEA, ASAINI MWAKA MMOJA

Drogba baada ya kurejea kundini.
Didier Drogba wakati akifanyiwa vipimo (kushoto). Kulia akisaini mkataba wa mwaka mmoja Chelsea.
Jembe ndani ya Stamford Bridge.
STRAIKA wa Ivory Coast, Didier Drogba amejiunga na klabu yake ya zamani Chelsea kwa kusaini mwaka mmoja.
Drogba mwenye umri wa miaka 36 amerejea Stamford Bridge baada ya kuondoka klabuni hapo miaka miwili iliyopita na kwenda klabu za Shanghai Shenua na Galatasaray.
Akiwa klabu ya Shanghai Shenua, Drogba alicheza mechi 11 na kufumania nyavu mara 8 huku akiifungia Galatasaray mabao 15 baada ya kucheza mechi 37.
Mkali huyo wa kucheka na nyavu anarejea Chelsea aliyoifungia mabao 100 katika mechi 226 alizoichezea tangu alipojiunga mwaka 2004 kwa pauni milioni 24 akitokea Marseille.
Staa huyo ameeleza kuwa asingeacha fursa ya kufanya kazi na kocha wake wa zamani Jose Mourinho.
"Ilikuwa ni uamuzi rahisi - nisingeweza kuacha fursa hii ya kufanya kazi na Jose kwa mara nyingine. Kila mmoja anaelewa uhusiano wangu na klabu ya Chelsea ulivyo na mara zote namekuwa nikijihis hapa ni nyumbani" - Alisema Drogba baada ya kutua darajani

Tuesday, 22 July 2014

Rodriguez atua Bernabeu kwa miaka 6

Real Madrid imemnunua James Rodriguez
Mshambulizi wa Colombia na Monaco James Rodriguez amezunduliwa kama mchezaji wa Real Madrid baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka 6 na mabingwa hao wa bara Ulaya.
Mchezaji huyo wa aliyetwaa taji la mfungaji mabao mengi katika kombe la dunia huko Brazil ameandikisha kandarasi ya miaka 6 na klabu hiyo.
Duru zinaiarifu BBCMichezo kuwa huenda James akapokea kitita cha dola milioni mia moja.
Kutua kwake huko Bernabeu kumemuweka Rodriguez katika mizani sawa na Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.
Real Madrid imemnunua James Rodriguez
Iwapo Rodriguez atalipwa takriban pauni millioni 80 basi huenda atakuwa mchezaji wa nne ghali zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Suarez.
Rodriguez aligonga vichwa vya habari baada ya kutinga mabao 6 licha ya timu yake ya Colombia kubanduliwa nje ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali.
Rodriguez alifunga mabao dhidi ya Ugiriki , Ivory Coast na Japan lakini atakumbukwa zaidi kwa bao lililopigiwa upatu kuwa bora zaidi katika mashindano hayo dhidi ya Uruguay.
Kabla ya kujiunga na Monaco Rodriguez alikuwa amedhihirisha udeddea wake huko Ureno alikotwaa mataji matatu ya ligi akiwa na klabu ya Porto.
Real Madrid imemnunua James Rodriguez
Naibu mwenyekiti wa wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev alisewaambia wanahabari kuwa klabu hiyo haikuwa na niya ya kumuuza mshambulizi huyo lakini hawakutaka kupitwa na kitita kikubwa kilichotolewa kwao na kumweka katika mizani sawa na washambulizi ghali zaidi katika hstoria ya kandanda.
Madrid ilitoa kitita cha pauni milioni 80 kumnunua Ronaldo alipotokea Manchester United mwaka wa 2009.
Na ulimwengu na kandanda ulipodhania kuwa historia hiyo haingevunjwa Madrid ilitoa pauni milioni 85.3m mwaka uliopita na kumnunua Bale kutoka kwa Tottenham ya Uingereza.

Steven Gerrard astaafu soka

Steven Gerrad astaafu soka
Nahodha wa England na club ya Liverpool Steven Gerrard hatimaye ametundika daruga kuichezea timu ya taifa lake la England akiwa na miaka 34. Gerrard amejiimarisha kwenye kikosi cha uingereza tangu mwaka 2000 walipoipiga Ukraine kwa mabao mawili kwa nunge.
Kiungo huyo wa Liverpool amesema aliufurahia muda wote alipoichezea timu ya taifa na kwa kweli ni siku ya masikitiko kwake.
Hivi sasa Gerrard atakuwa katika nafasi za juu za ubalozi katika chama cha soka cha England.
Anastaafu akiwa amecheza michuano mikubwa sita na kufunga mabao 21. Na hivyo kushika nafasi ya tatu baada ya Peter Shilton na David Beckam.

DUNGA ACHUKUA MIKOBA YA SCOLARI KUINOA BRAZIL


Kocha mpya wa Brazil, Dunga.
Mchezaji wa zamani wa Brazil, Carlos Caetano Bledorn Verri 'Dunga', amepewa mikoba ya kukinoa kikosi cha Brazil baada ya kocha Luiz Felipe Scolari kujiuzulu. Dunga amepewa kikosi hicho kilichoboronga katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika nyumbani kwao huku timu hiyo ikiambulia nafasi ya nne. Kikosi hicho pia kilipata dhahama baada ya kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya mabingwa wa kombe hilo Ujerumani katika mechi ya Nusu Fainali.



ERASTO JOSIAH TOGA


James Rodriguez akifanyiwa vipimo mjini Madrid kujiunga na Real Madrid.
Rodriguez wakati akitoka hospitali mjini Madrid baada ya kukamilisha vipimo.…

Rodriguez wakati akitoka hospitali mjini Madrid baada ya kukamilisha vipimo.
Rodriguez akionyesha dole ndani ya Madrid.
MPACHIKA mabao wa Kombe la Dunia 2014, Mcolombia, James Rodriguez, ametua katika klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania kwa dau la pauni milioni 60.
Staa huyo amesaini mkataba wa miaka sita na mabingwa hao wa Klabu Bingwa Barani Ulaya kwa msimu wa 2013/2014.
Rodriguez ambaye tayari amefanyiwa vipimo, anakuwa mchezaji wa nne kwa uhamisho ghali baada ya Gareth Bale aliyesajiliwa kwa pauni milioni 80 sawa na Cristiano Ronaldo kwenda Real Madrid, Luis Suarez uhamisho wa pauni milioni 75 kwenda Barcelona.