Kundi la wapiganaji wa Kiislam
la Boko linatuhumiwa kuendesha mapigano kaskazini mwa Nigeria na katika
mpaka wa Nigeria na Cameroon.
Maofisa wa polisi nchini Cameroon wamesema kuwa
ndege za kivita na vikosi vya kijeshi vimepelekwa karibu na mpaka wa
Cameroon baada ya tukio la kutekwa kwa mke wa mwanasiasa maarufu ambaye
pia ni naibu waziri mkuu Amadou AliKiongozi mwingine wa kidini Seini Boukar Lamine anadaiwa kutekwa na wapiganaji hao wa Boko Haram huku mapigano yakiripotiwa kuendelea katika eneo hilo.
Katika mji wa kaskazini mwa mji wa Kano imearifiwa kuwa wane wameuawa katika milipuko miwili inayodaiwa kutekelezwa na kundi la Boko Haram.
Sherehe za kukamilisha mfungo wa Ramadhan zimefutwa kaskazini mwa Nigeria mwaka huu kutokana na hofu ya usalama.
No comments:
Post a Comment