Mourinho : Drogba ni Chelsea damu
Mourinho : Drogba ni mChelsea damu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .
Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa
miaka 36 aliwahi kushinda mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia
mwaka wa 2004-2012 kabla ya kuguria Galatasaray.Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.
Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .
Drogba akiwa Galatasaray.
Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013.
No comments:
Post a Comment