MMOJA AFARIKI DUNIA, WATANO WAJERUHIWA AJALINI TARIME LEO
Hii hajari imetokea leo ikihusisha gari la ZACHARIA EXPRESS lililokua likitokea TARIME
MTU mmoja, Fatuma Juma Kitumbo (35), amefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali mbaya ya basi la Zakaria Express lenye namba za usajili T 405 CLT lilipoanguka katika eneo la Sen'gensa Kijiji cha Remagwe, Kata ya Nyamaraga, Wilaya ya Tarime mkoani Mara leo.
Marehemu huyo ambaye ni mtoto wa dada yake
mpiga picha wa ITV Musoma, Ahmad Kitumbo, alikuwa akitokea nchini Kenya
akielekea jijini Mwanza. Imeelezwa kuwa sababu ya kifo chake ni kutokwa
na damu nyingi kutokana na ajali hiyo mbaya.
Ajali hiyo ambayo imethibitishwa na Jeshi
la Tarime na Rorya na Kamanda wake Razalo Mambosasa, ilitokea kati ya
saa 2.00 hadi 3.00 asubuhi.
Ilidaiwa kuwa chanzo chake ni dereva wa
basi hilo kumkwepa binti mmoja aliyekuwa na ngo'mbe wa kukokotwa na
jembe na lori lililokuwa barabarani, ndipo basi hilo likaanguka na
kusababisha maafa hayo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri
ya mji wa Tarime, Roberty Onesmo alithibitisha kutokea kwa kifo hicho
na aliwataja majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo kwa matibabu kuwa
ni dereva wa basi hilo Mbaraka Shamsi (35) aliyeumia kifua, Roberty
Nashoni (28) aliyeumia kichwani na mkewe Bhoke Roberty Nashoni (28),
aliyeumia kifuani na kichwani, Selfina Abuo (44), Lucy Ngure (22).
Hata hivyo, alisema Bwana Nashoni na mkewe
wana hali mbaya na wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Musoma kuchunguzwa
na kwa matibabu zaidi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilayani hapa,
Amos Sagara Nyabikwi aliwatembelea majeruhi wa ajali hiyo katika
hospitali hiyo na alifanikisha kuwasafirisha majeruhi hao kupelekwa
Hospitali ya Musoma.
IMETOKA GLOBAL PUBLISHER
No comments:
Post a Comment