DUNGA ACHUKUA MIKOBA YA SCOLARI KUINOA BRAZIL
Kocha mpya wa Brazil, Dunga.
Mchezaji wa zamani wa Brazil, Carlos Caetano Bledorn Verri
'Dunga', amepewa mikoba ya kukinoa kikosi cha Brazil baada ya kocha
Luiz Felipe Scolari kujiuzulu. Dunga amepewa kikosi hicho kilichoboronga
katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika nyumbani kwao huku
timu hiyo ikiambulia nafasi ya nne. Kikosi hicho pia kilipata dhahama
baada ya kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya mabingwa wa kombe hilo Ujerumani
katika mechi ya Nusu Fainali.ERASTO JOSIAH TOGA
No comments:
Post a Comment