MAOFISA WA MALAYSIA WAKABIDHIWA VIFAA VYA KUTUNZA KUMBUKUMBU YA NDEGE ILIYOLIPULIWA
Mwanajeshi
wa wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi akikabidhi mojawapo ya vifaa vya
kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia MH17
iliyolipuliwa kwa maofisa wa Malaysia.
Vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia vilivyokabidhiwa.…
HATIMAYE wapiganaji wanaoiunga mkono Urusi wamekabidhi vifaa viwili
vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege MH17 ya Malaysia
iliyolipuliwa kwa maofisa uchunguzi wa Malaysia huko Ukraine.Vifaa viwili vya kutunza kumbukumbu (black boxes) vya ndege ya Malaysia vilivyokabidhiwa.…
Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa ni baada ya wito mbalimbali kutolewa kuhusu maofisa wa uchunguzi kuruhusiwa kufanya uchunguzi wao eneo hilo la ajali iliyouwa watu 298.
Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak ameeleza kuwa vifaa hivyo vilikabidhiwa mjini Donetsk jana baada ya mazungumzo ya muda mrefu na wapiganaji hao.
No comments:
Post a Comment