Saturday, 26 July 2014

Tambwe na mgomo baridi Simba SC

Straika wa kimataifa wa ya Simba, Mrundi, Amissi Tambwe,
Martha Mboma na Ibrahim Mussa
BAADA ya siku nne kutoonekana mazoezini imebainika kuwa straika wa kimataifa wa ya Simba, Mrundi, Amissi Tambwe, alikuwa na mgomo baridi akiushinikiza uongozi kumlipa fedha zake za usajili.
Awali iliripotiwa kuwa straika huyo aliyefunga mabao 19 msimu uliopita na kunyakua kiatu cha dhahabu, alikuwa amefiwa na shangazi.
Chanzo cha habari kutoka ndani ya klabu hiyo kilisema kuwa, mshambuliaji huyo aliamua kususia mazoezi akishinikiza kumaliziwa fedha zake za usajili alizokuwa akiidai timu hiyo.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, hata hivyo mchezaji huyo amelipwa pesa yake, kilichobaki kwa sasa ni kuongezewa mshahara na marekebisho kadhaa katika mkataba wake na wamemuahidi kuanza kumlipa mwakani ndiyo maana juzi Alhamisi alianza mazoezi.
“Tambwe alikuwa na mgomo wala hakusafiri kama ilivyodaiwa, alikuwa kalala tu nyumbani kwake tangu Jumamosi iliyopita akishinikiza kumaliziwa fedha zake za usajili, kapewa chake ndiyo maana unamuona mazoezini,” kilisema chanzo hicho.

No comments:

Post a Comment