GARI LA DUDE LAKAMATWA DAR KWA UJAMBAZI
Read More
GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ, lilikutwa likiwa na…
Stori: waandishi wetu
GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
Gari la dude muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ,
lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya
Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za
usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
Inadawa kuwa muda mfupi baada ya kukamatwa, Dude alitokea Polisi na
kulitambua gari lake, lakini maelezo yake hayakuwatosheleza Polisi hivyo
kumshikilia katika kituo kidogo cha Polisi Mabatini hadi kesho yake
alipodhaminiwa.Waandishi wetu walifanya jitihada za kumtafuta Dude ili azungumzie taarifa hizo, lakini aliwataka kufuatilia jambo hilo katika kituo cha Polisi, akisema suala hilo lipo mikononi mwao.
Shauri linalomkabili msanii huyo limefunguliwa kwa Jalada namba .KJL/RB/6399/14 UNYANG’ANYI
IMETOKA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment