LOO! Mwanafunzi wa Chuo cha T.I.A tawi la mkoani Singida, Moza Kasim Mohemed (20) ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejichoma kisu tumboni kwa madai ya kuchoshwa na usaliti wa mpenzi wake aitwaye Joel ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho.
Tukio hilo la kushangaza lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 10, mwaka huu maeneo ya Jovena katika Hosteli za Miami ambapo Moza alikuwa akiishi na mpenzi wake huyo.
Chanzo chetu kilidai kuwa, siku hiyo muda mfupi kabla ya tukio hilo kulitokea kutoelewana kwa wawili hao ambapo majirani walimsikia Joel akimtuhumu Moza kwamba amekuwa msaliti na anahisi ana simu nyingine ya ziada ambayo anaitumia yeye akiwa hayupo.
Timbwili lilisikika kwa muda mrefu kiasi
kwamba ilibidi majirani waanze kuchungulia dirishani na wakamsikia Moza
akimwambia Joel kwamba, kwa vile hamwamini hadi anafikia kumpiga bora
ajichome kisu afie mbali.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Joel naye alisikika
akimjibu Moza kwa kumwambia kama dhamira yake ni hiyo, basi ajichome
tu.
Akiwa hospitalini baada ya kutolewa kisu tumboni.
Malumbano hayo yaliendelea kuchukua ukurasa mpya ambapo Joel
aliendelea kumpa kibano na baadaye alimuacha na kutoka nje, baada ya
dakika chache zikasikika kelele za ajabu kutoka kwa Moza ambapo majirani
ambao ni baadhi ya wanafunzi wenzake wakatoka na kuingia chumbani na
kumkuta akigalagala na damu zikimvuja huku kisu kikiwa tumboni.“Hawa watu walikuwa na tabia ya kukwaruzana mara kwa mara na Joel alikuwa akimpiga yanaisha ila siku hiyo ilikuwa ni mzozo wa hatari, baada ya tukio watu walijaa lakini kila mtu akawa anaogopa kumgusa Moza, Joel alipata ujasiri yeye na rafiki yake wakambeba na kumkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Singida,” kilisema chanzo.
Kikaendelea: “Jana (juzi Jumapili) tulikwenda hospitali kumsalimia, tulikuta ameshatolewa kisu na ameshashonwa, hali yake inaendelea vizuri, ila habari ya mjini Singida kwa sasa ni juu ya tukio hilo, hata tulipofika hospitali tulikuta wanafunzi wengi.”
No comments:
Post a Comment