Friday, 17 October 2014

VAI WA UKWELI: SIPIKI, NAMSTAREHESHA MPENZI TU!



MSANII wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ametoa kali ya mwaka kwa kusema kuwa, licha ya kwamba sifa ya mwanamke ni kujua kumpikia mume mahanjumati, yeye hana muda wa kupika ila anajua jukumu lake ni kumstarehesha mpenzi wake tu.

Msanii wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Vai alisema hawezi kutumia muda wake kupika awapo nyumbani kwani kazi hiyo hufanywa na hausigeli.
“Mimi nikiwa nyumbani sipiki, mpenzi wangu akija kwangu tutanunua chakula, tutakula kisha tutaendelea na mambo yetu lakini siwezi kuingia jikoni kupika, kazi hiyo atafanya hausigeli,” alisema Vai.

No comments:

Post a Comment