Saturday, 4 October 2014

SIMBA YABANWA MBAVU HATARI

Kiungo wa Simba SC, Shaban Kisiga (kushoto) akimtoka beki wa Stand United, Reyna Mgungira.
SIMBA SC imelazimishwa sare ya tatu mfululizo nyumbani baada ya kufungana bao 1-1 na Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, tayari timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba SC wakitangulia kupitia kwa Shaban Kisiga dakika ya 35 kabla ya Stand United kusawazisha dakika 10 baadaye.
Wafungaji  ni Shaban Kisiga kwa Simba SC na Kheri Mohamed wa Stand United.
Kikosi cha Simba SC: Hussein Sharrif ‘Cassilas’, Miraj Adam, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joram Mgeveke, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/Said Ndemla dk46, Shaban Kisiga ‘Malone’/Amri Kiemba dk84, Emmanuel Okwi na Ibrahim Hajibu/Elias Maguri dk68.
Kikosi cha Stand United:John Mwenda, Swaleh Abdallah, Yassin Mustafa, Iddi Mobby, Peter Mutabuzi, Omar Mtaki, Mussa Said, Reyna Mungira, Kheri Mohamed, Soud Mohammed/Salum Kamana dk70 na Suleiman Jingo.

No comments:

Post a Comment