MBUNGE wa Bihalamuro, Dk. Anthony Mbasa (CHADEMA), amesema kamwe
serikali haiwezi kufanya jambo lolote la maana kama itashindwa kuongeza
pensheni za wazee na kuwalipa kwa wakati.
Dk. Mbasa alitoa kauli hiyo alipokuwa akichangia katika hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2014/15.
Alisema kuwa ni aibu kwa serikali kushindwa kuwalipa wazee wastaafu pensheni zao kwa wakati, licha ya kuwa pensheni hizo ni kidogo.
Mbali na hilo, alisema pamoja na kuwa wapo wazee wastaafu ambao walikuwa ni wanajeshi na wengine walishiriki katika mapambano ya vita vya Kagera, lakini bado wastaafu hao ni kama hawathaminiwi.
Akizungumzia vyanzo vya mapato ambavyo serikali haiviweki wazi, alisema yapo mazao ya mistu ambayo yanaweza kutumiwa vizuri na kwa uaminifu taifa linaweza kuongeza kipato.
Alihoji kuwa fedha hizo zinazotokana na mazao ya mifugo zinaenda wapi, kwani ni fedha nyingi ambazo zinapatikana, lakini serikali imekuwa ikifumba macho na kuzitumia bila kuzitolea maelezo.
Pamoja na mambo mengine, aliishambulia serikali kwa kufanya mambo yake kwa ubabe hususani wananchi wenye uwezo mkubwa na kuwaacha wale wenye uwezo mkubwa.
Dk. Mbasa alisema inawezekanaje serikali ikawa kila siku inachoma vyavu za wafugaji ambazo zinasemekana zina macho madogo bila kufanya utafiti zinakopatikana.
“Serikali hii ni ya ajabu sana inasikitisha kuona kila siku wavuvi wadogo wanakimbizwa na kuchomewa nyavu zao kwa kisingizio kuwa zina macho madogo, lakini cha kujiuliza nyinyi viongozi mbona hamjawahi kujiuliza nyavu hizo zinatengenezwa wapi?” alihoji Dk. Mbassa.

No comments:
Post a Comment