WANANCHI wa
kada mbalimbali nchini, wamewataka wanasiasa kuacha kutumia mchakato wa
Katiba Mpya Inayopendekezwa kusababisha vurugu, migogoro na machafuko
kwani nafasi ya kuendeleza amani na utulivu uliopo bado ipo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, baadhi ya wadau wamesema dalili zinaonyesha kuwa huenda kukawa na hali ya sintofahamu wakati zoezi la upigaji wa kura za maoni likielekea kufanywa wakati wowote kuanzia hivi sasa.
John Katiti aliyejitambulisha kama mwanaharakati za haki za binadamu, alisema Katiba Mpya Inayopendekezwa ina baadhi ya mambo ambayo ni mazuri na mengine hayana masilahi kwa umma, hivyo wanasiasa wanatakiwa kulichukulia jambo hilo kwa tahadhari kubwa wakati wakijadili hatima yake.
“Katiba Mpya Inayopendekezwa imeshakuwa vita ya wanasiasa, kila mtu anataka wananchi wasikilize maoni yake. Ni wakati mgumu sana kwa watu wa kawaida, ni rahisi kwao kudanganywa na kujikuta wakichukua hatua ambazo zinaweza kututia majaribuni siku za mbele, hakuna sababu ya kuingia katika mgogoro kwa sababu nchi yetu bado ina amani,” alisema.
Mdau mwingine anayetokea Chama Cha Wanasheria Tanzania, aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema hatua iliyofikiwa katika mchakato wa Katiba Mpya Inayopendekezwa, ni yenye kuhitaji umakini mkubwa kwa wanasiasa, kwa sababu kauli na matendo yao yanaweza kusababisha machafuko.
“Ukitazama mchakato mzima ulivyokwenda, tokea bungeni, ulikuwa na mpasuko. Ingawa kisheria katiba pendekezwa ni halali, lakini kama tunavyojua, umekosa maridhiano kwa maana hiyo kuna makundi ya watu wanaopingana juu ya ubora wake, ipo haja ya kuendelea kutumia busara kwenye mjadala kuelekea kura ya maoni, tusije kufikia hatua ya watu kuanza kuhamasisha uasi dhidi ya kundi lingine, bado taifa limeshikamana, wanasiasa lazima walitazame hili,” alisema.
Katiba Mpya Inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa Marais Jakaya Kikwete na Mohamed Shein wa Zanzibar hivi karibuni baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Bunge Maalum la Katiba lililomaliza kazi yake Oktoba 4, mwaka huu mjini Dodoma.

No comments:
Post a Comment