Kim Martin ameiambia mahakama kuwa Pistorius "anahitajika kulipa kwa kile alichotenda."
Upande wa mashitaka unajenga hoja kwamba Pistorius mwenye umri wa miaka 27 ahukumiwe kifungo jela.
Upande wa utetezi umekuwa upendekeza kuwa Pistorius atumikie adhabu ya kifungo cha nyumbani na kufanya kazi za kijamii kwa kosa hilo- pendekezo ambalo limetajwa na mwendesha mashitaka Gerrie Nel kuwa "si sahihi na linatisha".
Upande wa mashitakam umesisitiza kuwa Pistorius lazima afungwe jela, wakisema vitendo vyake vya kizembe vimesababisha "familia kupata pigo kubwa".
'Hatulipizi kisasi'
Katika kikao cha kusikiliza mwenendo wa hukumu hiyo, Bi Martin amesema ana hofu na Pistorius.
"Familia yangu si ya watu wanaOtaka kulipiza kisasi, tunahisi kwamba kumpiga mtu risasi nyuma ya mlango ambaye tena hana silaha, unahitaji adhabu ya kutosha, amesema.
Jumatano, Bi Martin alielezea kuumizwa kwake aliposikia mwanamitindo huyo wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 29 aliuawa kwa kupigwa risasi, akisema kifo chake "ulikuwa mwisho wa dunia".
No comments:
Post a Comment