Friday, 19 December 2014

NATAFUTA MWANAUME WA KUZAA NAYE.


Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ Penniel Mwingilwa amesema sasa anatamani kuzaa lakini tatizo lipo kwa mwanaume wa kuzaa naye.

Tuesday, 2 December 2014

SHEKHE AFA AKIZIKA




Aliyekuwa Shehe Mkuu wa Bakwata Wilaya ya Mbeya, Abubakar Mketo amefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita  kufuatia kuanguka ghafla makaburini wakati akitoa mawaidha ya Kiislam ya jinsi waumini wanavyotakiwa kuishi katika ulimwengu wa dhambi! Inauma sana!

MVUA ILIYONYESHA JIJINI MWANZA YASABABISHA MAFURIKO


Daraja likifurika maji baada ya mvua kubwa kunyesha asubuhi ya leo jijini Mwanza.

Sunday, 30 November 2014

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFANYA KWELI TUZO ZA CHANNEL O NCHINI AFRIKA KUSINI

Diamond Platnumz akipozi baada ya kutwaa tuzo tatu za Channel O jana usiku nchini Afrika Kusini.…

MAMLAKA HUSIKA YASHAURIWA KUTENGUA UTEUZI WA PROF TIBAIJUKA, PROF MUHONGO, JAJI WEREMA NA MASWI




Waziri wa Madini na Nishati, Profesa Sospeter Muhongo.
WABUNGE kwa pamoja wamekubaliana kuondoa maazimio 12 yaliyoletwa bungeni na Kamati ya PAC na kuleta maazimio mapya 8 ambayo yamekubaliwa.

Thursday, 6 November 2014

AMA KWELI MCHEPUKO SIYO DILI


MH! ‘Haga gangi’ (haya mengine)!  Simon Manase (22) ambaye ni dereva wa bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Nguyami, wilayani Gairo mkoani hapa amecharangwa mapanga mwilini na kukatwa mkono wa kulia na mtu aliyetajwa kwa jina la Frank akidai kumfumania na mkewe vichakani.

BASI LAGONGA TRENI NA KUUA IFAKARA


Basi la Super Aljabir baada ya ajali.

Sunday, 2 November 2014

FUMANIZI LA MWALIMU



   
KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.

Tuesday, 21 October 2014

MSANII YP AFARIKI DUNIA

Taarifa niliyoipata hivi punde inahusiana na msiba wa aliyekuwa mkali wa Bongo Fleva, YP kutoka kundi la wanaume Family.
Babu Tale

PISTORIOUS AFUNGWA MIAKA 5

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

MADENTI WALIWA MIGUU NA MAMBA


WANAFUNZI wawili wa shule za msingi za Nyabisara (Murito) na Kerende Kata ya Kemambo wilayani Tarime, Mara wameumwa hadi kuondolewa nyama zao za miguu na mamba walipokwenda kuoga maji ya mto kwa nyakatitofauti.

MBONGO ACHOMWA VISU SAUZI


WIVU wa mapenzi bwana! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la David Patrick Chagu (pichani) aliyekuwa akiishi Jimbo la George nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’  amekumbwa na mauti kwa kuchomwa visu na mpenziwe aliyefahamika kwa jina moja la Monica.

ANASWA AKITEKA DENTI



HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.

KOMANDO WA JWTZ AUA KISA MAPENZI


INAUMA sana! Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiuaga mwili wa Aron Kihundwa (28) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar walijikuta wakidondoka na kuzimia kufuatia uchungu wa kumpoteza mpendwa wao huyo aliyedaiwa kuuawa na Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Octavian Mgowele.
Aron Kihundwa akiwa mahututi hospitali kabla ya kifo chake.

MSANII MWINGINE AFARIKI

Msanii nyota wa filamu nchini Sherry  Charles Magali akiwa hoi hospitalini Wodi Namba 8 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro katika picha hii iliyopigwa na mwandishi wetu Ijumaa iliyopita, Okt 17, 2014.

HAAA! MBOWE



Kiongozi wa Kambi ya Upinzani (Bungeni), Freeman Mbowe, wiki iliyopita alipamba vilivyo mitandao ya kijamii, haikuwa kwa sababu ya tishio la maandamano kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wala Katiba Mpya, ‘topiki’ ilikaa kimapenzi zaidi.

Friday, 17 October 2014

DIAMOND AIBU NYINGINE DODOMA!


KWELI ni aibu nyingine! Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Jumamosi iliyopita alikumbwa na aibu nyingine kufuatia onesho lake kufanyika ndivyo sivyo na hivyo kuzua tafrani miongoni mwa mashabiki wake mjini hapa.

UZINDUZI MAALUM WA NGUO ZA T.I WATANGAZWA DAR

Rappa kutoka nchini Marekani, Clifford Joseph Harris,'T.I' ni mmoja wa wanamuziki watakaopiga shoo katika Usiku wa Fiesta 2014 viwanja vya Leaders Club.  

HUKUMU YA PISTORIUS YAINGIA SIKU YA NNE

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius (kulia) akitembea ndani ya mahakama. Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius anatakiwa kupewa 'adhabu ya kali' kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp, binamu yake Steenkamp ameliambia jopo la mahakama inayosikiliza hukumu yake mjini Pretoria.

MADAI MAZITO: MCHUNGAJI ATOROSHA MKE WA MTU!

MCHUNGAJI anayejiita nabii na mtume, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) aliyetajwa kwa jina moja la Emmanuel amejikuta ndani ya majanga kufuatia madai mazito kwamba amemtorosha mke wa mtu ambaye ni mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo anayekuja juu kwa kasi, Janet Mrema.

SIRI NZITO ZAFICHUKA TRAFIKI WA MAHABA


BAADA ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’ ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.

UCHAGUZI MSUMBIJI: RENAMO HATUTAMBUI MATOKEO

Kiongozi wa Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO, Alfonso Dlakama (katikati).
Chama cha kikuu cha upinzani nchini Msumbiji cha RENAMO kimetoa yake ya moyoni kuwa hawatayakubali matokeo yajayo ya uraisi na ubunge pamoja na serikali za mitaa.

WATAKA KATIBA ISIWE CHANZO CHA MIGOGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya M.Kikwete
WANANCHI wa kada mbalimbali nchini, wamewataka wanasiasa kuacha kutumia mchakato wa Katiba Mpya Inayopendekezwa kusababisha vurugu, migogoro na machafuko kwani nafasi ya kuendeleza amani na utulivu uliopo bado ipo.

MISS TANZANIA 2014 UTATA MTUPU


Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo.
Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji.

MAMA AMNG'ATA ULIMI SERENGETI BOYS




HATARI! Katika hali isiyotarajiwa, mwanamke mmoja aliyefahamika kama Mama Abuu amefanya tukio la ajabu baada ya kumng’ata na kumkata ulimi kijana Paulo Simon mwenye umri wa miaka 18, kufuatia ‘Serengeti Boy’ huyo kukataa kufanya naye mapenzi katika eneo la Tindigani, Kimandolu mjini Arusha hivi karibuni.

VAI WA UKWELI: SIPIKI, NAMSTAREHESHA MPENZI TU!



MSANII wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ ametoa kali ya mwaka kwa kusema kuwa, licha ya kwamba sifa ya mwanamke ni kujua kumpikia mume mahanjumati, yeye hana muda wa kupika ila anajua jukumu lake ni kumstarehesha mpenzi wake tu.

LULU: BONGO MOVIES ISHABUMA


STAA wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kwa mtazamo wake anaona Bongo Movies imebuma hivyo ameamua kukomaa na shule ili awe na kitu kingine tofauti na sanaa.

Tuesday, 14 October 2014

HALIMA MDEE NA MATESO YA SEGEREA



MBUNGE wa Jimbo la Kawe jijini Dar na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Halima James Mdee ambaye aliwekwa Mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar kwa saa kumi na mbili amesimulia mambo matano mazito aliyokumbana nayo hali iliyomfanya atokwe machozi.

DENTI AJICHOMA KISU KISA MAPENZI


LOO! Mwanafunzi wa Chuo cha T.I.A tawi la mkoani Singida, Moza Kasim Mohemed (20) ambaye ni mkazi wa jijini Dar es Salaam, amejichoma kisu tumboni kwa madai ya kuchoshwa na usaliti wa mpenzi wake aitwaye Joel ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho.

UTEKAJI WA WATOTO DAR WATIKISA JIJI


LICHA ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kupitia kwa kamanda wake, Camillius Wambura kutumia nguvu kubwa kukanusha kwamba, hakuna matukio ya utekaji wa watoto wadogo, hasa wanafunzi, lakini matukio hayo YAPO!!

MAMA KANUMBA, LULU NDANI YA FILAMU MPYA IITWAYO 'MAPENZI YA MUNGU'

Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo 'MAPENZI YA MUNGU' ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.

Saturday, 4 October 2014

Mtoto wa kizazi cha 'msaada' azaliwa

Mwanamke mmoja nchini Sweden amejifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa bila kizazi kabla ya kuwekewa kizazi cha mwanamke aliyekuwa katika miaka yake ya sitini.

Muingereza mwengine akatwa kichwa

Alan Henning kushoto mda mchache tu kabla ya kukatwa kichwa na mtu aliyesimama kando yake.

BIRTH DAY YA DIAMOND WEMA AWA GUMZO

NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.

MSIBANI KWA ALI CHOKI

Ndugu na majirani wa karibu wakiwa katika msiba wa mke wa Ali Choki, Shuwea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya kuugua kwa muda mrefu na kuaga dunia usiku wa kuamkia leo.

SIMBA YABANWA MBAVU HATARI

Kiungo wa Simba SC, Shaban Kisiga (kushoto) akimtoka beki wa Stand United, Reyna Mgungira.

UTAPELI MZITO KWA OBAMA

Taasisi…

Utapeli mzito umeshamiri Bongo ambapo imebainika kuna taasisi iliyojipachika jina la Tanzania Loan Society inayojieleza kuwa inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa Serikali ya Marekani huku ikiwarubuni watu kuwa inatoa mikopo bila riba.
NI Gumzo! Hiyo ndiyo kauli pekee inayoweza kuakisi pati ya kuzaliwa ya supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ametimiza umri wa miaka 25, iliyofanyika usiku wa kuamikia jana kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF), Posta jijini Dar, Risasi Jumamosi lilikuwepo ndani ya nyumba.

Thursday, 2 October 2014

Mwanasheria Mkuu Z’bar azikataa ibara 22 Katiba


Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman.
“Kwa hiyo kama Serikali haikuwa na msimamo kwa maana ya upande, maana yake ni ipi pengine unisadie… nilipiga kura kwa kuzingatia utashi wangu na maoni yangu.”

Waliopiga kura ya hapana walalamika kutishwa


Wahudumu  wa Bunge Maalumu la Katiba wakiwa wamebeba masanduku ya kura za wajumbe waliopiga kura za siri kwa Sura ya 11 hadi 19 ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Dk. Mbasa aionya serikali

MBUNGE wa Bihalamuro, Dk. Anthony Mbasa (CHADEMA), amesema kamwe serikali haiwezi kufanya jambo lolote la maana kama itashindwa kuongeza pensheni za wazee na kuwalipa kwa wakati.
Dk. Mbasa alitoa kauli hiyo alipokuwa akichangia katika hotuba ya bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2014/15.

Kura za Z’bar ni pasua kichwa


Mwenyekiti wa Bunge la katiba Samweli Sitta akizungumza Bungeni Dodoma jana.PICHA|MAKTABA 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

BETHIDEI YA WASTARA TAMU, CHUNGU


BETHIDEI ya msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma imegeuka kuwa maumivu baada ya kumkumbuka aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ukumbini.

KAJALA AMSHTAKI MAMA WEMA!


KIMENUKA! Habari ya mjini kwa sasa ni bethidei ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutimiza miaka 26 tangu kuzaliwa, lakini ndani ya tukio hilo, mengine yameibuka!

Tuesday, 30 September 2014

KIGWEMA, BEST NASSO: TUTAKUKUMBUKA SIDE BOY


Wasanii Best Nasso kushoto, Hamisi Kibiti ambaye ni Meneja wa Best Nasso na kulia ni msanii Kigwema kwenye picha ya pamoja wakiwa safarini kuelekea Lindi kwenye mazishi ya msanii mwenzao.

KABURI LA RECHO LALOA MACHOZI!


Roho inauma! Kwa mara nyingine, kaburi la aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Rachel Leo Haule ‘Recho’ (pichani) limeloa machozi ya mastaa wakati wa kusimikwa msalaba baada ya kujengwa na kuonekana la kisasa, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.

MILIONEA WA JWTZ ALIVYOUAWA KWA RISASI



NI taharuki iliyojaa majonzi na simanzi kufuatia Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU jijini Dar kuondokewa na mpiganaji wake, Sajenti Yohana  Lugendo Gweso (40) ambaye alikuwa milionea aliyepigwa risasi sita mwilini na kufariki dunia papo hapo.

PAKA AFUGWA HIRIZI MTINI


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.

NILISHUHUDIA NIKICHOMWA MOTO


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.

SEREMALA AJINYONGA, AACHA MASWALI


KATIKA hali ya kushangaza, mtu mmoja ambaye ni fundi seremala aitwaye Emmanuel Carlos, mkazi wa Kwabinyau Magomeni jijini Dar amekutwa akiwa amejinyonga saa mbili asubuhi Septemba 23, mwaka huu katika kile kinachodaiwa kuchoshwa na mgogoro wa kifamilia.