Bintou Schmill a.k.a 'The Voice' baada ya kumchapa Mirjana Vujic kwa K.O.
Bintou akizichapa na…
Bintou Schmill a.k.a 'The Voice' baada ya kumchapa Mirjana Vujic kwa K.O.
Bintou akizichapa na Mirjana.
BONDIA maarufu wa kike Mwafrika aishiye barani Ulaya, Bintou Yawa
Schmill, mkazi wa Ujerumani Septemba 26, mwaka huu alitwaa taji la
ubingwa wa ngumi za kulipwa unaotambuliwa na IBF.Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake Mirjana Vujic kwa K.O katika raundi ya tatu.
Pambano hilo lilionyeshwa live kupitia Euro Sport na kutazamwa na maelfu ya watu walioshuhudia bondia huyo wa kike Mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radi.
Bintou Schmill (30) a.k.a The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,.
Baada ya pambano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Stadthalle/Saalbau Frankfurt-Nied, Bintou alitangazwa kuwa bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani Ulaya na kuvikwa mkanda unaotambuliwa na IBF.
No comments:
Post a Comment