MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard
Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa
kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa
alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko
Segerea.
Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.
“Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao walitutilia shaka wakaanza kutupekua.
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,
No comments:
Post a Comment