Amani! Wakati mumewe Sunday Demonte akidaiwa kuwa yuko mbioni kuhukumiwa kwenda jela huko Dubai, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson amenaswa laivu kimahaba nchini Marekani akiwa na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Kassim Mganga.
“Tunashangaa kumuona Aunt ameambatana na mume wa mtu na huko anakoenda pia tunasikia watakuwa wawili tu na Kassim, inatutia shaka kwa kweli,” alisema mmoja wa ndugu wa mume kwa sharti la kutoanika jina lake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo nchini Marekani, wawili hao walitia maguu hivi karibuni kwa mwaliko maalum wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo Kassim alipewa nafasi mbili hivyo akaamua kumchukua Aunt.
“Kassim aliambiwa atafute kampani ya kuja nayo huku ndipo akaona Aunt anafaa kwa kuwa mwenyewe amedai ni mtu wake wa karibu,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kwamba, baada ya wawili hao kufika nchini humo, walipanga katika hoteli moja kisha kuanza kujiachia kwenye viwanja tofautitofauti wakila bata ndani ya Jiji la New York.
Baada ya mwanahabari wetu kunasa mchapo huo, alimtafuta Aunt kupitia WhatsApp hakupatikana, bahati nzuri Kassim alipatikana na kusema:“Tumekuja kwa mwaliko wa ubalozi wetu, Aunt ni mshkaji wangu kwa hiyo usishangae sana nikila naye bata,” alijibu Kassim.
No comments:
Post a Comment