Wasanii
Best Nasso kushoto, Hamisi Kibiti ambaye ni Meneja wa Best Nasso na
kulia ni msanii Kigwema kwenye picha ya pamoja wakiwa safarini kuelekea
Lindi kwenye mazishi ya msanii mwenzao.
Mdogo
wa msanii Side akiwa kwenye picha ya pamoja na Best Nasso, Kigwema na
waombolezaji wengine mara baada ya kufika mkoani Lindi.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Best Nasso na Kigwema wamefunguka
kuwa daima watamkumbuka msanii mwenzao, Side Boy aliyefariki mapema jana
kwa upungufu wa damu katika Hospitali ya mkoa wa Lindi.
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu wakiwa njiani
kuelekea msibani mkoani Lindi, wasanii hao walisema kuwa watamkumbuka
marehemu siku zote kwa kuwa walikuwa marafiki wakubwa ndani na nje ya
muziki na kuongeza kuwa ni msanii pekee aliyekuwa akiimba nyimbo zenye
meseji zenye kugusa maisha ya watu kwa kujali zaidi ujumbe na siyo soko
kama wanamuziki wengine.
“Hakuna neno tutakaloweza kusema kuelezea hisia zetu. daima
tutamkumbuka Side Boy kama msanii mwenzetu, rafiki na kaka yetu. RIP”
No comments:
Post a Comment