KUFUATIA kutoa kipigo cha mabao 2-0 kwa timu ya Yanga, Klabu ya Mtibwa Sugar
imesema kuwa straika wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santos ‘Jaja’
atachemka katika ligi ya Bongo, na kusisitiza ni busara kama
wangemuandalia mapema nyaraka zake ili arejee kwao kuendelea na majukumu
mengine.
Kitendo cha Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mtibwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kimeendeleza ‘uteja’ wa timu hiyo kwenye uwanja huo kwani mara ya mwisho kwa Yanga kuibuka na ushindi uwanjani hapo ilikuwa Septemba 19, 2009 ikiwa chini ya kocha, Dusan Kondic.
Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru, ameliambia Championi Jumatano kuwa mwaka huu wamedhamiria kurudisha heshima yao ya miaka ya nyuma kwa kuwa wana uzoefu wa ligi na wameanza hilo kwa kuipoteza Yanga huku akiongeza kuwa straika huyo ni wa kawaida, hawezi kusumbua katika ligi, ni bora akarudishwa kwao kuliko ‘kuchota’ mamilioni ya Yanga.
“Msimu huu Mtibwa tumedhamiria kurudi katika heshima yetu tuliyoipata mwaka 1999 na 2000 kwa kubeba kombe na kulionyesha hilo, tumeanza kwa kuibabua Yanga na Jaja wao.
“Maana kila mara ilikuwa ni Jaja, Jaja huyu Jaja ndiyo nani? Amefichwa na mabeki imara, hakuonekana kabisa uwanjani.
“Ni straika mwenye umbo zuri na siyo uwezo uwanjani, unajua timu zetu hizi zinaamini watu kutoka nje wana uwezo kuliko vijana wa hapa, kitu ambacho si sahihi.
“Wanavuna pesa tu wakati hapa kuna vijana wenye uwezo mkubwa wa kusaidia timu. Wawarudishe tu kwao watafute mastraika wa kweli Bongo,” alisema Kifaru ambaye amekuwa Ofisa Habari wa Mtibwa tangu mwaka 1996.

No comments:
Post a Comment