Roho inauma! Kwa mara nyingine, kaburi la aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Rachel Leo Haule ‘Recho’ (pichani) limeloa machozi ya mastaa wakati wa kusimikwa msalaba baada ya kujengwa na kuonekana la kisasa, Ijumaa Wikienda lilikuwepo.
Walipofika makaburini, mastaa hao walijikuta wakiangua vilio huku baadhi yao wakizimia kwa kumkumbuka mpendwa wao.
Tofauti na mastaa wengine, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Blandina Chagula ‘Johari’ walipitiliza kwa kulia kwa sauti kubwa.
Kuna wakati Odama alishindwa kuvumilia kulisogelea kaburi kwani aliangua kilio kilichosababisha mama wa Bongo Muvi, Herieth Chumila kumzuia kwa kuhofia kuishiwa nguvu.Mwisho, Odama na aliyekuwa mchumba wa Recho, Saguda George walitoa neno la shukrani kwa watu wote waliofika eneo hilo na kuomba ushirikiano kwa lolote litakalotokea.
Nayo familia ya Recho, iliwapongeza Odama na Saguda kwa kuwa na moyo wa upendo kwa marehemu tangu alipoumwa mpaka alipoaga dunia hadi kumjengea kaburi na kuwaomba waendelee kushirikiana kwa ajili ya umoja waliounganishwa na Recho.
Mbali na Odama, Johari, Herieth na Saguda, baadhi ya mastaa wengine ni pamoja na Steve Nyerere, Mike Sangu, Najma, Lamata, Kupa na wengine kibao.Recho (26) alifariki dunia Mei 25, mwaka huu wakati ajikifungua ambapo kichanga chake nacho kiliaga dunia.
CHANZO;GLOBAL PUBLISHERS.
No comments:
Post a Comment