Karibu mpenzi msomaji kwenye blog hii, ili tuweze kuhabarishana na kubadilishana mawazo juu ya masuala ya MICHEZO SIASA ELIMU, MAISHA na mengineyo ndani na hata nje ya Tanzania. Simu :+255655534913/ +255764547675 Barua pepe :erastotoga@gmail.com
Tuesday, 30 September 2014
Monday, 29 September 2014
Friday, 26 September 2014
NI SHEEDA! MUIGIZAJI WA FILAMU SLIM ADAIWA KUGOMA KUREJESHA GARI
Sto
NI sheeda! Muigizaji wa filamu za Kibongo, Salim Omary ‘Slim’ amejikuta akiwekwa nguvuni katika Kituo cha Polisi cha Makangarawe, Yombo-Buza, jijini Dar akidaiwa kugoma kurejesha gari aina ya Land Lover Discovery walilopewa zawadi siku ya ndoa.
Gari
hilo walipewa na wakwe zake alipofunga ndoa na binti yao aitwaye Asia
Morgan, mwaka jana lakini ilipofika Mei mwaka huu (takriban miezi tisa
tu ndani ya ndoa), wawili hao walitengana na kusababisha wakwe hao
wageuke mbogo kudai chao kwa maelezo kwamba walitoa zawadi hiyo kwa
binti yao hivyo kwa kuwa wametengana, wanataka chao.NI sheeda! Muigizaji wa filamu za Kibongo, Salim Omary ‘Slim’ amejikuta akiwekwa nguvuni katika Kituo cha Polisi cha Makangarawe, Yombo-Buza, jijini Dar akidaiwa kugoma kurejesha gari aina ya Land Lover Discovery walilopewa zawadi siku ya ndoa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Asia alifikia uamuzi wa kwenda kuishi nyumbani kwao Tegeta, jijini Dar baada ya kushindwa kuvumilia tabia ya wivu wa kupindukia aliyokuwa nayo Slim.
“Baada ya kutengana wazazi wa msichana huyo
walimwambia Slim awakabidhi gari moja kwa kuwa anayo mawili na kama
anataka Discovery (Land Lover) wamuachie lakini wapate moja kwa ajili ya
binti yao kuendea chuo,” kilisema chanzo.
Akizungumza kwa jazba, mama mzazi wa Asia alisema, walimzawadia gari
hilo kwa kuwa wote walikuwa wanapenda tasnia ya filamu hivyo gari hilo
lingemsaidia yeye na mume wake katika shughuli zao.“Kinachouma ni kwamba tusingefikishana hapa lakini tulishamuomba sana Slim kurudisha gari hilo au ampe mwanetu gari lingine abaki na hilo kama analipenda lakini alikataa na mbaya zaidi ana kila kitu, kuanzia ufunguo na kadi ya gari kitu ambacho hatendi haki kwa mtoto wetu,” alisema mzazi huyo.
kizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa, mzazi huyo alisema licha ya Slim kwenda Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kushtaki ili arudiane na binti yao, haitawezekana.
“Nashindwa kuelewa kabisa jambo hili nilijitahidi sana kulivumilia lakini nimeona imeshindikana kabisa hivyo tuliamua kwenda nyumbani na kumchukua kumfikisha kituoni hapa maana sisi tulimfanya kama mtoto wetu lakini yeye amekuwa mkaidi,” alisema mama huyo.
Mwandishi wetu alimfuata Slim kituoni hapo na kuzungumza naye kuhusiana na sakata hilo ambapo alisema anachofahamu yeye ni kwamba zawadi inapotolewa kwenye harusi na wazazi inakuwa ni ya mke na mume lakini anawashangaa wazazi hao kuidai ikiwa hata mkewe hajampa talaka.
“Nashindwa kuelewa kabisa kwa sababu wazazi wa mke wangu walitoa gari lile kama zawadi sasa sielewi kwa nini walidai tena wakati mke wangu sijamuacha, suala hili lipo Bakwata.
“Isitoshe, gari hilo nimelitengeneza sana mpaka kufikia lilivyo sasa kwani bado lipo gereji, lakini kwa kuwa wameamua kunidai, baada ya miezi mitatu nitakuwa nimewapa gari lao,” alisema Slim.
Thursday, 25 September 2014
Jaja atakiwa kuondoka nchini
KUFUATIA kutoa kipigo cha mabao 2-0 kwa timu ya Yanga, Klabu ya Mtibwa Sugar
imesema kuwa straika wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santos ‘Jaja’
atachemka katika ligi ya Bongo, na kusisitiza ni busara kama
wangemuandalia mapema nyaraka zake ili arejee kwao kuendelea na majukumu
mengine.
Wednesday, 24 September 2014
Kocha Mcameroon awapa Yanga ubingwa
Tuesday, 23 September 2014
Obama aapa kuangamiza Islamic State
Rais wa Marekani Barack Obama
amesema Marekani itashambulia kundi linalojiitaa Islamic state kote
nchini Syria na Iraq ili kuwanyima kabisa makao ya kujificha .
MWALIMU AKUTWA AMEFUNGWA MINYORORO KANISANI
Ndugu
wa mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35)
ambaye ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa
la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko
Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo kwa miezi
nane mfululizo.
Subscribe to:
Posts (Atom)