Ni kwa sababu wananchi hawatoi ushirikiano
unaotakiwa kwa wana-usalama, jambo linalosababisha kazi ya kuwabaini
wauaji kuwa ngumu.
Hussein Machozi
Serikali yenyewe ndiyo inawapa nguvu wauaji, na sisi inatufumba macho tu kuwa inawafuatilia. Rushwa kwa vyombo vinavyohusika na mauaji ya albino pia ni tatizo, serikali yenye nguvu ndiyo sababu ya hao wenzetu kufa mimi na wewe hatuna nguvu ya kuzuia hata robo.
Coletha
Serikali haiwezi kushindwa kwa sababu wao ndiyo wenye kila
kitu, polisi, jeshi usalama wa taifa na mahakama ni yao, sasa hapo
wanashindwaje? Kama siyo udhaifu, tena wa makusudi dhidi ya wananchi
katika utendaji kazi, wao ndiyo wenye wajibu wa kuwalinda wananchi wao.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_u9d69K1AqPV6GKBcz_5qJGxIR43qran9QIomIPEbecgfU_99zWJz59_m-YcWBrGM631BQvY50-Ieto7l0j5xu29K_IHJSdRHm3yFZTxAvygCVVSFSPDXGWdeZ0flQ8DH_EIsxuNIWFBIx3oUb69R90a17vpCZsM0JlKvECOqu4h3Et6TRmPGNkY46fLZNT993AztfDEvGMtEwEcvlnus3MeOF5eo0AP0vhgrdOftlEi2pG_drbiI9w-0lLSnwhJg=s0-d)
William Mtitu.
Mimi napendekeza atakayemkata mkono mmoja
albino akishikwa akatwe mikono 2 na mguu mmoja ili iwe fundisho.Lakini
pia itolewe elimu ya kutosha kuwa huwezi kutajirika kwa kiungo cha
albino, kama kuna mtu anaamini anaweza basi aliyekamatwa na kiungo
apelekwe baharini au ziwani avue samaki aone kama atavua samaki wengi,
mahakama zitoe hukumu mapema zinapochelewesha maamuzi, ukatili na mauaji
unaendelea.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vGeuFi88TL2N2GTkAUDhUyFdJJG0vXVJjYhz2K3SDMB5GzeT_uNnr2cbJjrnbhCEJ3vHmpydp0V54Z68FiujC1RWXg0JBgnEv2rr0UW2LjG_EJ2AXI53dCAxJ63ps8YalTbNen-gjjbaj-f8KidB8tTqRwFgJdTCaq5cyUMgq8Tluuh1Z63Twp5aNUkvhJMzGfcVMhccqFofaXEa4qS8ZFku9YwgPQJbRjB4K8mpaKTs0CHyXbObuWOw=s0-d)
Bi Mwenda
Wanawaonea sana, kwa kweli tangu wameanza kuwaua hakuna mabadiliko
yoyote ya kimaendeleo waliyopata, pengine hata hao wanaopaswa kuzuia nao
ni wahusika ndiyo maana kuna ugumu.
No comments:
Post a Comment