Thursday, 4 September 2014

YANGA YATEMBEZA KIPIGO KENYA

Mshambuliaji wa timu ya Yanga SC, Geilson Santana Santos 'Jaja' (kushoto) akimtoka beki wa timu ya Thika ya nchini Kenya, Simon Mbugua (kulia) jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki. Yanga SC ilishinda 1-0.

Jaja akishangilia baada ya kuipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 58 kipindi cha pili.
Wachezaji wa timu ya Yanga SC, Mbuyu Twite (wa kwanza kushoto), Haruna Niyonzima (katikati), Geilson Santana Santos 'Jaja' (wa pili kutoka kulia) na Oscar Joshua (wa kwanza kulia) wakishangilia bao la Jaja.
Mashabiki wakifuatilia mechi ya Yanga SC dhidi ya Thika ya nchini Kenya.
Kiungo wa Yanga SC, Andrey Coutinho akimtoka mchezaji wa Thika, Michael Olunga.
Said Bahanuzi wa Yanga (kushoto) akimtoka mchezaji wa Thika.
Wachezaji wa timu ya Thika David Kingatua na Tonny Kizito wakijadiliana jambo kabla ya kupiga mpira wa faulo.
Kikosi cha timu ya Yanga SC.
YANGA SC jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Thika ya nchini Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwenye mechi ya kirafiki.


IMETOKA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment