Mesut Ozil wa Arsenal
Mechi hiyo ndio itakayofungua rasmi msimu mpya wa ligi kuu nchini humo.
Arsenal itajibwaga uwanjani ikiwa na wachezaji wapya waliosajiliwa kama vile Alexi Sanchez,lakini pia ikikumbuka kichapo cha mabao sita kwa tatu ilichopata dhidi ya mabingwa hao.
Hatahivyo baada ya kushinda taji la F.A kuna motisha kubwa katika uwanja wa Emirates msimu huu.
Yaya Toure Mancity
Vilevile hakuna mchezaji wa kilabu hiyo aliyewasili kutoka likizo ya kombe la dunia wiki iliopita ambaye atashirika katika mechi hiyo huku mshambuliaji Alvaro Negredo akiendelea kuhudumia jeraha lake la mguuni.
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Goroud huenda akakosa kushiriki baada ya kushindwa kutamba wakati Arsenal ilipochuana na Monaco katika kombe la Emirates.
No comments:
Post a Comment