Liverpool yailaza Mancity
Liverpool iliwalaza mabingwa wa
ligi kuu ya Uingereza Manchester City mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti
timu hizo zilipokutoshana nguvu 2-2 katika muda wa kawaida katika
mechi ya kirafiki ya kuwania taji la mabingwa wa kimataifa
(International Champions Cup).
Mechi hiyo iliyovutia mashabiki elfu 50,000
katika uwanja wa yankee ulioko New York ilianza bila ya msisimko
kipindi cha kwanza kikikamilika matokeo yakiwa ni suluhu bin suluhuLakini katika kipindi cha pili, mabingwa hao walidhibitisha niya yao mapema kupitia bao la Stevan Jovetic.
Kiungo cha kati wa Liverpool ,Jordan Henderson aliisawazishia timu yake kabla ya Jovetic kuirejeshea City uongozi .
Uongozi huo hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu kwani Raheem alifanya mambo kuwa 2-2.
Waandalizi waliamua mechi hiyo ikamilishwe kwa kupiga matuta ya penalti.
Na hapo vijana wa Brendan Rodgers walitamba na kujikatia tikiti ya nusu fainali ambapo sasa watachuana na AC Milan ya Italia .
City sasa itakwaruzana na Olympiakos ya Ugiriki.
Mchuano huo unajumuisha timu 8 za kimataifa.
No comments:
Post a Comment