Friday, 22 August 2014

REAL MADRID WATUA BONGO


Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati) akizungumzia namna Timu yake ilivyojiandaa kuwakabili Wakali hao wa soka Duniani wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es Salaam.Kulia ni Luis Figo na kushoto ni Fernando Sanz Duran ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
Mchezaji Kiongozi wa Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid,Luis Figo akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ujio wao hapa nchini.Figo amewaahidi wa Tanzania kuwa yeye na Wenzake watatoa burudani kabambe katika Uwanja wa Taifa jijini Dar hapo kesho.
Mchezaji Fernando Sanz Duran (kati) nae akitoa maneno yake kuhusu mchezo huo.
Mwanasoka Christian Karembeu akizungumza.

No comments:

Post a Comment