Mateka 15 wa Kikurd wanaoshikiliwa na wapiganaji wa ISIS.
SAA chache baada ya kuuwa wanajeshi 300 wa Syria, Kundi la wapiganaji wa ISIS limetoa onyo lingine kwa Marekani likiachia video inayowaonyesha mateka 15 wa Kikurd ambao nao watauawa iwapo Marekani haitaondoa majeshi yake.
ISIS wamesema wataendelea kuwachinja mateka hao mpaka Marekani itakapoondoa majeshi yake.
Katika video hiyo, Kundi la ISIS linaonekana likimchinja mmoja wa
mateka hao wa Kikurd waliokamatwa wakati wa mapigani nchini Iraq.
Wapiganaji
wa ISIS wakiwaswaga wanajeshi zaidi ya 200 waliokamatwa katika ngome ya
anga ya Tabqa nchini Syria katika jangwa kuelekea eneo la mauaji.
No comments:
Post a Comment