Chanzo hicho kimesema kuwa Wanajeshi wa Kikurdi wanajaribu kusafisha eneo lenye madini na mabomu ya kutegwa ambayo yameachwa mahala hapo na kikundi cha wapiganaji wa himaya ya kiislamu. Mashambulizi yao ya chini ya ardhi yamekuwa yakiunganishwa na msaada wa vikosi vya askari wa Marekani ambao wanatoa ulinzi wa anga.
Taarifa ya wizara ya ulinzi ya Marekani imesema makundi kumi na nne ya wanamgambo hao yametimuliwa mchan wa jumapili na ndege za kivita za Marekani zikiwemo zile zisizo na rubani.
Usiku wa kuamkia leo Ikulu ya Marekani imesema itaendelea na mashambulizi ya anga kama ilivyoamuriwa na Rais wa nchi hiyo Barack Obama, ikiwa ni mkakati wa sera ya Marekani ya kulinda watu na mali zake zilizopo Iraq.
Maafisa wa White House wamesema bwawa lililo kombolewa ni muhimu kwa maji na umeme na kwamba endapo lingeachwa kwa wanamgambo hao na kulifumua kingo zake lingesababisha mafuriko kwenye mji wa Mosul na pengine hadi jijini Baghdad mahala ambapo kuna ubalozi wa Marekani.
Waziri wa mambo ya nje wa Iraq anayeondoka madarakani Hoshyar Zebari ameiambia BBC Mjini Baghdad kuwa wapiganaji wa himaya ya kiislamu wameleta changamoto kubwa kwa Iraq na kwamba ni tishio kwa dunia.
No comments:
Post a Comment