Wema akiwa na Diamond
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua
hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie
harusi.
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka
hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es
Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia
hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie
harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu
kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu
ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani
waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa
sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta
umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya
Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya
ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku
zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi
Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine
uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda,
hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na
kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali
huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi
kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma
sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu
siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi
kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao
nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi
yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha
baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake
huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini
hatujaachana na hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.
“Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao.”
No comments:
Post a Comment