Vyombo vya habari vya Uchina vinasema kuwa watu kama 150 wameuwawa na wengi kujeruhiwa.
Shirika la Marekani linalochunguza ardhi linasema kitovu cha tetemeko hilo la kipimo cha 6.1 kilikuwa kwenye eneo la mbali la milima katika jimbo la Yunnan.
Wakuu wa huko wanasema majengo mengi yameangamia,pamoja na nyumba na shule na mawasiliano yameathirika sana.
Watu walihisi tetemeko hilo piya katika majimbo ya jirani ya Guizhou na Sichuan.
Eneo la kusini-magharibi la Uchina liko katika kanda inayotingishwa mara kadha na mitetemeko.
Tetemeko lilotokea Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu maelfu kadha.
No comments:
Post a Comment