Friday, 1 August 2014

JOSE CHAMELEONE ATUA BONGO, KUPAGAWISHA MAISHA CLUB

Chameleone akitoka uwanja wa ndege kuelekea kwenye gari.
…Akiwa na wenyeji wake waliofika kumpokea.
…Akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ukumbi wa New Maisha Club anayejulikana kwa jina la HK.
…Akitaniana na wenyeji wake.
MWANAMUZIKI kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone, alitua Dar es Salaam jana saa mbili usiku tayari kwa kufanya shoo ya nguvu leo katika ukumbi wa New Maisha Club uliopo Masaki jijini Dar.
Akizungumza na mtandao huu muda mfupi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Chameleone alisema kuwa amekuja Bongo kuwapagawisha watu kiburudani hivyo mashabiki wake wafike kuona vitu vyake vipya.

No comments:

Post a Comment