Thursday, 14 August 2014

HAPA LAZIMA UCHEKE!


MTU mmoja alifariki na kwenda jehanamu.

Kufika huko akakuta kuna jehanamu tofauti
tofauti kwa kila nchi. Akaamua kuzunguka
zunguka ili aweze kuipata jehanamu yenye
maumivu kidogo zaidi.
Akaiendea jehanamu ya Ujerumani. Akamwuliza
mtu aliyemkuta mlangoni. "Wanakufanyajeukiingia humu?"
Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka kwenye kiti
cha umeme kwa saa moja, kisha wanakulaza
kwenye kitanda cha mizumari kwa saa moja
nyingine. Kisha anakuja shetani wa Kijerumani
anakucharaza bakora kutwa nzima."
Mtu huyo hakuipenda kabisa jehanamu hiyo.
Akaamua kujaribu jehanamu za Marekani,
Uingereza, Urusi na nyinginezo nyingi. Lakini
akagundua kuwa zote zina adhabu sawa tu na
jehanamu ya Ujerumani.
Kisha akaifikia jehanamu ya Tanzania.
Akastaajabu kuona kuna foleni ndefu kweli ya
watu wakisubiri kuingia humo. Kwa mshangao
usiosemekana akauliza, "Jamani kwani humu
wanawafanyaje?"
Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka kwenye kiti
cha umeme kwa saa moja, kisha wanakulaza
kwenye kitanda cha mizumari kwa saa moja
nyingine. Kisha anakuja shetani wa Kitanzania
anakucharaza bakora kutwa nzima."
Akazidi kustaajabu. Akauliza, "Lakini mbona
kinachofanyika humu ni sawa kabisa na
kinachofanyika kwenye jehanamu zingine, sasa
kwa nini hapa kuna foleni kubwa sana watu
wote wanakimbilia huku?"
Jamaa mmoja akamshika mkono. Akamvutia
pembeni. Akamnong'oneza, "Watu wanakimbilia
huku kwa kuwa jehanamu ya Tanzania haina
umeme wa uhakika, unakatika katika kila
dakika kwa hiyo kiti cha umeme hakifanyi kazi.
Halafu pia misumari ilishalipiwa lakini wala
haijaletwa na mzabuni kwa hiyo kitanda cha humu ni raha tu kukilalia. Na jambo jingine ni kuwa shetani wa Kitanzania alipokuwa duniani alikuwa mtumishi wa umma. Kwa hiyo ameshazowea kufika ofisini na kusaini kitabu cha mahudhurio na kisha kuondoka zake
kwenda kufanya shughuli zake binafsi."

No comments:

Post a Comment