Friday, 1 August 2014

Jaja Vs Zahir ni shiida, Maximo awaamua mara 3

Beki Rajab Zahir (kulia) dhidi ya Genilson Santos ‘Jaja’ (kushoto), wamekuwa na kazi ya ziada mazoezini.

KWELI Yanga imepania kufanya kweli, kila mchezaji anataka kuonyesha uwezo wa juu, lakini ushindani huo umesababisha upinzani kuwa mkali kwa wachezaji wa timu hiyo, beki Rajab Zahir dhidi ya Genilson Santos ‘Jaja’, ambapo wamekuwa na kazi ya ziada mazoezini.
Jaja, raia wa Brazil, ameonekana kupata wakati mgumu kila anapokuwa akikabwa na Zahir kiasi cha kufikia wawili hao kukwaruzana zaidi ya mara moja katika siku tofauti, hali ambayo imesababisha kocha wao mkuu, Marcio Maximo kuingilia na kuwapa maelekezo zaidi ya mara moja pia.
Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola jijini Dar, Jaja alionyesha ufundi lakini Zahir alikuwa mgumu na hakutaka kukubali kupitwa kirahisi, hali hiyo ilisababisha kuchezeana kibabe mara kadhaa, ambapo kuna muda alimkwatua kiasi cha Jaja kutolewa nje na kupatiwa huduma ya kwanza.
   Kocha wao mkuu, Marcio Maximo akiingilia na kuwapa maelekezo zaidi ya mara moja pia.
Jana pia kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini, Zahir alipewa jukumu la kumdhibiti Jaja ambapo shughuli ilikuwa pevu, baada ya muda mambo yakawa kama ya juzi.
Wakiwa katikati ya mazoezi, Zahir alimkwatua Jaja kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kitendo kilichosababisha Jaja kukasirika na kumvaa beki huyo, lakini kabla ya kumfanya chochote, Maximo aliingilia na kusimama kati yao kisha kuanza kutoa maelezo kwa wote wawili.

IMETOKA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment