Friday, 22 August 2014

MASTAA WA REAL MADRID WALIVYOTUA JIJINI DAR

Baadhi ya mastaa wa zamani wa Real Madrid baada ya kutua nchini jana usiku.

Mastaa hao wakiongozwa na wenyeji wao baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar jana usiku.
Mastaa hao wakihojiwa baada ya kutua jijini Dar jana usiku.
Beki wa zamani wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa, Cristian Karembeu akihojiwa na wanahabari baada ya kuwasili.
Mastaa hao wakifurahia jambo.
BAADHI ya mastaa wa zamani wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania jana usiku wametua nchini Tanzania tayari kwa mechi yao dhidi ya kikosi cha nyota wa Tanzania, Tanzania 11 hapo kesho.
Mastaa hao waliotua tayari ni pamoja na Luis Figo, Cristian Karembeu huku wengine wakitarajiwa kuingia nchini leo.
Mechi ya mastaa hao itapigwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment