Sunday, 24 August 2014

TANZANIA YAPIGWA NA WAKONGWE WA REAL MADRID

Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Luis Figo akiwatoka wachezaji wa Tanzania Eleven wakati wa mechi hiyo.

Mfungaji wa mabao matatu ya Wakongwe wa Real Madrid, Ruben de la Red akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Tanzania Eleven.
KIKOSI cha wakongwe wa Real Madrid kimetoa kipigo cha 3-1 kwa wakongwe wa Tanzania 'Tanzania Eleven'.
Mechi hiyo imepigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Kikwete.
Mabao ya Real Madrid yote matatu yalifungwa na Ruben de la Red huku la Tanzania Eleven likipatikana kupitia kwa Roberto Rojas aliyejifunga wakati akijaribu kuokoa.

No comments:

Post a Comment