Bobby Williamson ni kocha wa Kenya
Kocha mpya wa Harambee Stars Bobby Williamson
Williamson ambaye aliwahudumu kama kocha wa Uganda Cranes kwa miaka mitano kabla ya kutimuliwa baada ya Cranes kushindwa kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika CAF mwaka wa 2013 amesema kuwa ni jambo la kujivunia kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya Harambee Stars .
Hata hivyo raiya huyo wa Scotland amesema kuwa bado ataendelea na majukumu yake katika klabu mabingwa wa ligi kuu ya Kenya KPL hadi pale shirikisho la soka la Kenya FKF litakapokubaliana na klabu yake ya Gor Mahia.
Williamson anatarajiwa kuiongoza Gor mahia katika mchuano wa baraza la soka kanda ya Afrika Mashariki na Kati baada ya kutwaa taji la taifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 18.
Kocha huyo Aliiambia BBC kuwa ni wakati shirikisho la soka la Kenya FKF lirejelee soka ya vijana chipukizi ilikuimarisha nafasi yake ya kuboresha matokeo yake kimataifa.
No comments:
Post a Comment