SERENGETI FIESTA 2014 YAANZA MWANZA KWA KISHINDO
Msanii
wa Bongo Flava, Linah Sanga (wa pili kushoto) na mkali wa muziki huo na
mshindi wa tuzo ya AFRIMMA 2014, Diamond Platinum (kushoto) wakifanya
vitu vyao katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza jana.
Staa
wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' (kushoto),
akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho
la kwanza la Tamasha la Serengeti Fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba
mjini Mwanza jana jioni. Serengeti Fiesta inadhaminiwa na Kampuni ya Bia
ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Young D, akifanya vitu vyake ndani ya Uwanja
wa CCM Kirumba, jana wakati wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,
lilipofanyika kwa mara ya kwanza mjini Mwanza jana.
Msanii wa Bongo Fleva, Mr Blue akikonga nyoyo za umati wa wakazi wa
Jiji la Mwanza waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kirumba katika Tamasha
la Serengeti Fiesta.
Wasanii wa kikundi cha Makamandoo wakiwa kazini wakati wa Tamasha la
Serengeti Fiesta la mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza
jana.
Meneja
wa Bia ya Serengeti, Rodney Rugambo (kulia) akibadilishana mawazo na
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba
wakati wa tamasha hilo.
Wasanii wa kundi la Tanikando Group kutoka Igoma, Mwanza nao
wakionyesha umahiri wao kupamba onyesho la muziki la Serengeti fiesta
uwanjani hapo jana.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani
wakishangilia baada ya kukongwa na burudani wakati wa Tamasha la
Serengeri Fiesta lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza jana. Maonyesho hayo yatafanyika katika mikoa 18 nchini.
No comments:
Post a Comment