Mshambulizi wa Ivory Coast na
Chelsea ya Uingereza Didier Drogba alirejea kwa kishindo Stamford Bridge
lakini kuwepo kwake haikuinusuru The Blues kichapo cha mabao matatu kwa
nunge (3-0 )dhidi ya klabu ya Werder Bremen ya Ujerumani.
Kipa machachari Thibaut Courtois alipewa fursa ya kushika kwenye lango huko Weserstadion.Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22-kutoka Ubeljiji alijiunga na Chelsea mwaka wa 2011 lakini amekuwa Uhispania kwa mkopo kwa timu ya Atletico Madrid.
Eljero Elia na Felix Kroos walifungia Bremen kupitia mikwaju ya penalti huku mkwaju wa kichwa kwa Ludovic Obraniak ikiisaidia timu hiyo inayoshiriki kwenye ligi ya Ujerumani Bundesliga kuandikisha ushindi.
Elia alifunga penalti ya kwanza baada ya John Terry kuugusa mpira katika eneo la lango huku Obraniak akimsababishia aibu kipa mpya Courtois alipoiweka Bremen kifua mbele mabao 2-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.
Chelsea iliambulia kichapo cha 3-0 mikononi mwa Werder Bremen.
Eden Hazard John Obi Mikel na Petr Cech pia walihuruhusiwa kucheza .
Toni Kroos alikamilisha kivuno hicho cha mabao alipofuma mkwaju kimiani dakika mija tu kabla ya mechi hiyo kukamilika.
No comments:
Post a Comment